SOMO KUHUSU MAJARIBU
USOMI : 1 Wakorintho 10:12-13 I. MAANA YA JARIBU: Jaribu ni kipimo cha imani kwa watu wote; na mwisho ya kujaribiwa kwako na ( Mungu, Shetani, Sifa au Cheo, Ahadi ya Mungu, Mwili yako yenye kutamani na Tamaa zitokazo katika Nafsi ya mtu ); ni mpaka kufa. Jaribu halijawa jaribu, mpaka linamufikisha mtu kwenye njia panda; mahali pa kuamuwa kama ataacha Imani ya Yesu Kristo, kama ataacha alicho kuwa anafanya au akigojeye au tena mtu aendeleye kuvumiliya ( yaani kuchukuwa maamzi sahihi ) . Na hicho ni kipindi kizito cha kukatisha sana tamaa! II. KAZI AU LENGO YA JARIBU MAISHANI MWETU Kwa somo hili, tutagusia sana maana ya jaribu kwa Wakristo: - Jaribu inakuja kuandaa mukristo kupokea baraka, kuinuliwa au kupandishwa cheo; alakini ni lazima mtu huyo ashinde jaribu ndipo hayo yatajitokeza ( Yakobo 1:12 ), ( Kumbukumbu la torati 8:16 ); - Jaribu inamusaidia mukristo kutengeneza mawasiliano au mahusiyano (re...