KITU CHA KUFANYA UNAPO KUTANA NA MAJARIBU MBALIMBALI MAISHANI
USOMI : 1 Wakorintho 10:12-13
I. KIINGILIO:
Kumbuka kuna jambo ambalo unatakiwa kufanya kusudi uvuke hivyo vipindi viguma vya majaribu, hata kama Bwana ka ahidi tayari kufunguwa mulango ili jaribu lipite, sababu ya uaminifu wake; lakini katika kitabu cha Luka Mtakatifu sura 9:11; imeandikwa “... Yesu aliwaponya waliyo kuwa na haja ya kuponywa”. Na Mithili 8:17 nayo ina sema: “Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona” Tena Yeremiya 33:3 Bwana anasema: "Niite, nami nitakuitikia..."
II. JAMBO LA KUFANYA
Jambo la kwanza:
- Usimunungunikiye Mungu wala mwanadamu; sababu manunguniko huwa inarudisha ahadi ya Mungu nyuma. Mfano ya wana Waisraeli jagwani toka inchini Misri kwenda Kanani (Hesabu 14:34-38; 1 Kor. 10:10);
- Chunguza sana maneno ya kinywa chako, ili usije ukakiri mazaifu wala kujilaani mwenyewe (Yakobo 3:10; Mwanzo 25:32 na Kutoka 30:19). Tena jifunze pia kuchunga siri ya maisha au huduma yako; sababu Shetani ni mujanja sana, anazungukazunguka kama simba akitafuta mbinu za kukuangamiza. (1Petro 5:8). Kwa hiyo usiwe mujinga kama alivyo fanya mfalme Hezekia, wakati wapelelezi walipo mujiya kutoka Babeli akidanganywa na zawadi, hadi kawafunuliya siri ya ufalme wake yote na kwa mwisho ikawa chukizo mbele za Mungu (Isaya 39:1-8);
- Usikasikirike na hata unge kasirika (sababu ni kawaida ya binadamu), ila usitambuke kipimo cha ma saa kumi na mbili (12h00) kwa siku sawa sawa na Neno la Mungu kwa kitabu cha Waefeso 4:26-27) sababu pia unaweza mupa sheteni mulango hata kutenda zambi. Tena Zaburi 34:7 nayo inasema: “Malaika wa Bwana hu fanya kituo, akiwazunguka wamchao na kuwaokoa” kwa hiyo si baraka kwako Mungu akija kwako usiku akutute ulilala na uchungu wala hasira moyoni mwako. Na tena kumbuka, Mungu wetu anataka tufurahi kila siku (Wafilipi 4:4);
- Usitafute musaada kwa wanadamu wala kujitangaza au kueleza shida zako kwa wanadamu: kuendea wafumu na kutafuta njia isiyo halali machoni pa Bwana ambaye ni Mungu wa wivu sana ( Kutoka 20:5) au tena kutafuta maisha au njia rahisi (raccourci) sababu kuna laana (Yer. 17:5-6).
Jambo la pili: NADHIRI AU DENI YA KAZI YA MUNGU (Zab. 50:14-15; Muhubiri 5:4-6).
- Chunguza vema ikiwa hakuna nadhiri ambayo hauja ondoa mbele za Mungu, sababu ni vema kujuwa ya kwamba uasi ni zambi mbele za Mungu na unapo kosa kuondoa nadhari yako, unahesabiwa kuwa muasi (1 Yoana 3:4);
- Uangaliye kama unazoweya kumushukuru Mungu anapo kutendea mema; sababu “...Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo” (Zaburi 33:1-4).
Jambo la tatu: KUTUBU
- Kwenda mbele za Mungu na moyo wa toba: kumbuka ya kwamba, kutubu ni zaidi ya maombi ya toba tena ni zaidi ya matengenezo wala kuhungama dhambi; sababu toba ina taka sana mabadiliko ya mutazamo, musimamo, hisia, tabiya, mwenendo, mawazo,... na bila uwezo na nguvu za Mungu ni vigumu mwanadamu mwenyewe abadilike au kubadilisha tabia yake mbaya (Yeremiya 13:23)
- Lengo la kutubu ambalo watu wengi haoni mara na mara wanapo tubu kwa Bwana; liko katika kitabu cha Matendo ya Mitume 3:19-20 na nilazima kukazana na maombi hadi upate Amani rohoni pia mabadiliko ya ndani; sababu Bwana hataki watu wake wapone majeraha yao kwa juu juu tu wakisema AMANI, Amani, wala hapana amani (Yeremia 6:14) ila anataka watu wake waburudishwe mioyo ili wawe na amani ya kudumu na wasiendeleye tena kujihukumu; kwa kuwa Yeye ni mfalme wa Amani (Waebrania 7:1-3) tena aligogomeya mashitaka yetu (original) musalabani kwa hiyo hatuna lazima ya kuendelea kujihukumu, soma (Wakolosai 2:13-14).
Jambo la inne: KUSHUKURU KWA IMANI PAMOJA NA KUTOA SADAKA
- Ni kumuonyesha Mungu ya kwamba bado unamutazamia na kumutegemea kusudi akuvushe ndani ya kipindi hiki kigumu ambacho huja wai pitiya hata siku moja. Kumbuka imani ni kuwa na uhakika ya mambo ya tarajiwao (Waebrania 11:1).
Kwa hiyo ni bora zaidi mkristo kumushukuru Mungu anapo pitiya vipindi vigumu tena vipya kwake; kwa malengo ya kutaka musahada wake yeye aliye kufikisha hapo ulipo.
Mfano ya vipindi ambavyo tunatakiwa kumushukuru Mungu kwa imani :
- Kufiwa na mzazi, mume, muke au mtu ambaye alikuwa tegemeyo kwako;
- Kuachwa na muchumba;
- Kufukuzwa kazini au kazi kufungwa;
- Biashara habiendi sawa (kihombo);
- Kumaliza masomo (diplôma);
- Kuolewa au kuowa;
- Kupata kazi mpya;
- Kuhamiya nyumba mpya,...
Hivyo vyote na vipindi vingine ni vipindi vipya na ni lazima kumualika Mungu aliye njia na mwenye kuifahamu vema. Ana sema katika kitabu cha Isaya 55:8 ya kwamba ...Mawazo na njia zetu si kama mawazo wala njia zake, asema Bwana!
Kwa kifupi, kumushukru Mungu kwa Imani (yaani ukiwa na matarajiyo au matumaini); inamugusa sana Mungu na kumupa nafasi ya kukushiriki katika kipindi kigumu na anakuwa musahada kwako. Sababu imeandikwa “kesho ya jua Mungu” soma Yakobo 4:13-16. Na hapo Mungu lazima akutiye nguvu ya kuingiya kwenye musimu (season) mpya.
Jambo la tano: KESHA SANA JU YA NDOTO UNAZO ZIOTA KITANDANI MWAKO
Neno la Mungu kwa kitabu cha Ayubu 33;14-17, inaeleza kwamba Mungu ana nena na watu wake kwa njia ya ndoto ili kuizuwiya nafsi yake isiende shimoni. Kwa hiyo unapopitiya ndoto aina hizi:
Mfano fulani ya ndoto zenye ujumbe ndani yake:
- Kuota uko shuleni au kwenye mutiyani;
- Kuota uko unapanda mlima mrefu;
- Kuota uko unaogeleya baharini au kuzama majini;
- Kupanda au kushuka ngazi (Escalier);
- Kuota uko kwenye njia panda au nyembamba sana hata kupita inashindikana au njia inafungwa;
- Ndoto kuhusu nyoka au umbwa;
- Kuchangiya chakula au kitanda na mtu aliye kufa;
- Kutembea kwenye matope na utelezi;
- Kuzini kwenye ndoto;
- Kukimbizwa na ngombe mwenye mapembe ;
- Ndoto ukiwa uchi;
- Ndoto ukipigwa mawe au kurushiwa mavumbi;
- Kutembeya miguu kanya;
- Kucheza mupira;...
Unapo pata ndoto kama na hizi, usizarau na kusema eti ni ndoto tu kama vile alivyo sema mfalme Farao (Mw. 41:6-7), maana kwa wakati huo, Mungu anajaribu kukusemesha na kukuonyesha ya kwamba uko kwenye shida na hauwezi shinda mwenyewe bila musahada wake. Kwa hiyo inakubidi kwenda mbele za Mungu na kufanya maombi ya toba na ya kushambuliya; huku ukiamini nakuitumiya damu ya Yesu Kristo ili ikuneneye mema (kukuombeya mbele za Mungu na katika ulimwengu wa roho) hata kama umefanya dhambi au kuna mashambulizi mbambali; usiogope wala kuwa na shaka, tumia tu hiyo damu ya Yesu kwa imani ili upate kuvunja au kufuta zile agano za kipepo katika ulimwengu wa roho zinazo bana maisha na nafsi yako isiendeleye sawasawa na mapenzi ya Mungu. Soma Waebrani 9:19-22; 12:24)
Umenielewa? Ikiwa hujaelewa, tafadhali fuatana nami tena katika mfululizo mwingine wa somo hili, siku chache zijazo. Tuzidi kuombeana. Ni mimi katika utumishi wa Kristo.
Pasteur Thaddée Bizy Barhazigirandi
UJUMBE WA NENO LA MUNGU KWA WATU WOTE
Umeletwa kwako na: KANISA "MULIMA WA MAKIMBILIO"
Communauté des Eglises Evangéliques pour toutes les Nations-Unies "C.E.E.N.U-BUKAVU"
N° 005, Av. Mulungulungu, Quartier Panzi, Commune d'Ibanda, Ville de Bukavu-RD Congo
à moins de 100 mètres sur RN 2
Adresse mail : tbizyma@gmail.com, thaddemabize@yahoo.fr
Facebook: Thaddée Barhazigirandi; Twitter: @ThaddeeBizimana
Linkedin: https://www.linkedin.com/in/thaddée-bizimana-b79301a8
.jpg)
Commentaires
Enregistrer un commentaire