KWA NINI MTU MWENYE THAMBI ANAPO AMINI YESU KRISTO, KIPATO CHAKE NI KAMA KINA ZOROTA?
USOMI : AYUBU 21:7-12; MALAKI 3:13-15; WAKOLOSAYI 1:12-17
I. KIINGILIO:
Lengo la somo hili, ni la kuimarisha yaani kuhimiza wapendwa katika Bwana, kuwatiya moyo na kuwapongeza; ili wasichoke kuomba na kutafuta kila siku uso wa Bwana; sababu Yesu Kristo anasema kuhusu kuridhi ufalme wa Mungu na mambo yake katika kitabu cha Matayo 11:12 ya kwamba: "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka" na (Wakolosai 1:13) inaeleza kwamba Mungu ; "Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.
Jambo la kufahamu sana ni kwamba tunapo amini Kristo Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yetu, kuna kitu ambacho tunasahau mara na mara (kwa kutojuwa au kwa kuzarau kutokana na mapokeyo ya kila mmoja wetu). Tunasahau kwamba:
- Yesu Kristo si
tu Bwana na Mwokozi, ila pia ni Mukombozi (rédempteur); sababu mtu anapokuwa thambini anakuwa akifuata na kuheshimu
sheria ya thambi kwa kuwa yeye ni mutumwa wa Shetani na anafanya mapenzi ya
baba yake Shetani aliye bwana wake. Sasa watu wengi wanapokea wokovu yaani, wanaokolewa
toka nguvu za giza (ufalme wa Shetani), na wanarizika tu na WOKOVU, wakasahau ya kwamba Kristo Yesu
hakuja na wokovu yenyewe ila pia alikuja na UKOMBOZI (rédemption) yaani alikuja kutulipia deni zetu kwa damu yake ya dhamani sana musalabani (1Wakor. 6:20); Damu inenayo mema
kuliko ya Abili (Waebr. 12:24) tena Yesu kaja kuturudishia vitu ambavyo Shetani
aliteka mateka kwetu au kutupokonya (1 Petro 1:18-20). Ndani ya Yesu kuna uzima wa milele na siyo tu wakutupeleka mbinguni, ila pia, tuishi maisha ambayo Mungu Baba alituandaliya tangu zamani hapa chini ya juwa ili tuweze kutembea kwenye kusudi lake ; "Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu..." Matendo ya Mitume 17:28.
-Kumbuka kwamba Yesu ndani ya Biblia anamutaja Shetani kama: Mwizi, Muuaji na Muharibifu (Yoana 10:10). Halafu mtu anapokuwa mutenda thambi hata kama angelifikiri na kusema eti "mambo yote ni salama" sababu ya uhuru wa kufanya thambi kwa kutimiza tamaa zote za mwili; akasahau ya kwamba Shetani hana rafiki wala si mwenye haki tena hasemi kweli; sababu yeye ni baba ya waongo; na ni sherti atimize hizo kazi zake, mtu anapo mukubali kama bwana wake;
- Kumbuka tena kama kuokoka ni kuzaliwa upya au mara ya pili kiroho soma Yoana 3:1-7; 2Wakorintho 5:17; 1Petro 2:2; Waebrania 5:11-14; Mathayo 18:3-4.
Kutokana na hiyo kweli ya neno la Mungu hapo juu; tunaona kama haiwezekani kabisa:
- kwanza : mtu aliye porwa mali na kuharibiwa kila kitu alichokuwa akifanya kwa kupata kipato na Shetani ambaye ni mwizi tena muuaji akaendelea vizuri bila musahada wa Mungu;
- pili: mtu huyo ambaye bado ni mugeni katika ufalme wa Mungu, bado mtoto mchanga kiroho au katika imani; akarizika tu kuzaliwa mara ya pili, bila kutaka huo ukombozi wa baraka zake na mafanyikiyo yaliyo ibiwa na kuharibiwa na mwovu Shetani; kwa njia ya toba mbele za Mungu kwa damu ya Yesu; pamoja na kumutaka Roho mtakatifu aliye: Mwalimu, Kiongozi, Msaada, Mwombezi,... (Yoana 14:16-18, 25-28); ili amukomalishe na kumuongoza kwa ngisi mtu asije akapokeya mapokeyo ya wanadamu au ya dini (Marko 7 :7-9 ; Wakolosayi 2 :8); Ni vigumu mtu kufanikiwa bila uongozi wowote au kuelekezwa na Mungu au mtu mwengine Mungu aliye mutumiya, kama alivyo fanyiwa Sauli kwenye njia ya Damaski kwa kumuongoza mbele ya Mtume Anania (Matendo ya mitume 9:5-22);
- tatu na la mwisho: je? Mtu ambaye alikuwa akiishi kwa kupata kipato kupitia biashara haramu, kazi isiyo kuwa halali mbele za Mungu (aliyekuwa akiishi kwa zuluma, corruption, wizi, ukorofi, uongo, uwasherati, aliyekuwa muuaji mwenye kupora mali ya watu, muchuruzi wa dawa za kulewa, aliye fanikiwa kwa kuingiya mikataba na nguvu za giza, aliyekuwa mupiga ramuli au muaguzi kama ule mjakazi wa kipindi cha Paulo na Sila kwenye kitabu cha Matendo ya mitume 16:16-19); mfano wa Zakayo aliye tubu kwa kurudisha kila alicho pokeya kwa zuluma na ufisadi mara inne kwa kila mtu aliye ibiya kodi, soma Luka 19:5-10). Mtu huyo, anaweza anza mbiombio, tena kwa wepesi kutengeneza kipato au namna ya kuishi, na tayari amesha haribu mazigira yake ya mbele ya mafanikiyo (bila tena kutegemeya soko yake ya zamani, wateja wake wa mbele, byashara yake ya zamani, marafiki na walezi au viongozi wake wa hapo zamani walio kuwa wakimuongoza kwenye kazi hizo tulizo zitaja hapo juu) pasipo msahada wa Mungu? Jibu ni hapana. Ndo maana, nilazima sana ku kaa na kwenda kwa bidii mbele za Mungu kwa toba, kwa kutaka uongozi mpya, njia nyipya (projects), marafiki na washirika wengine wapya; makusudi Mungu akufunguwe macho ya ndani uanze kuona opportunity zinazo kuwa mbele zako kwa wakati uliyo kubaliwa na Bwana ndani ya hiyo hiyo mazingira ya wokovu! Pasipo hiyo njia, mukristo atabaki akilalamika kama mtumishi Ayubu alivyo sema kwa kitabu cha Ayubu 21:7-12. Na wengine huacha wokovu na kurudi nyuma, ndani ya matope kama nguruwe anavyo fanya kisha kuoshwa au kurudiliya matapikiyo yao kama umbwa anavyo zoweya kufanya (2 Petro 2:20-22).
N.B1: Namupenda sana Mzee Nuhu, sababu
hakurizika tu kwa kuokoka yeye na jamaa lake kwenye garika na nvua ya siku 40 (chombo chake kikatuliya juu ya maji muda ya mwaka mmoja). Sababu, Nuhu alipotoka kwenye Safina,
alikuta kila kitu kimebadilika (hakuwa tena na majirani kama ilivyo kuwa kawaida; sababu watu wote walifariki na hayo
mafuriko, hapakukuwa tena soko, hakukuwa na shamba wala mimeya, hapakukuwa tena na serkali ambayo
angeliweza lilia shida yake, hakuna njia wala balabala,... Kila eneo ni matope mutupu) ; sasa ataanza je maisha hiyo mapya? Sababu ilikuwa musimu mpya kwake (new season sawasawa na kuokoka kutoka dhambini). Ikamubidi aende mbele za Mungu na zabihu
ambao kwa lugha ya kibiblia inaitwa MBEGU,
na hapo ndo Mungu alianza tena kurudisha tena kila kitu kwa nafasi yake (majira
yalikuwa yamebadilishwa yaani kipwa na nvua havikukuweko tena) ndipo Mungu akafanya kwa upya agano la
milele kuhusu dunia kwa kuapa kutoangamiza tena dunia tena kwa maji; akarudisha
majira ya kupanda, na kuvuna, ... kupitiya sadaka hiyo ya mbegu. Soma Mwanzo 8:13-17, 20-22. Hata wewe mwenyewe unaweza pia kujifunza kwa mzée Nuhu kwa kuanza kila kitu na sadaka hiyo ya mbegu; ili kumwalika Mungu awe Kiongozi, maana Yeye ana upako wa Alpha tena wa Omega tena ni Mungu mwenye Baraka zote.
II. JAMBO LINALO WAKWAMISHA WALIO WENGI ZAIDI SANA NI HILI:
Ø Jambo la kwanza: ni kukosewa na Malezi bora (Wazazi wa Kiroho au wa Imani)
Kuamini Yesu Kristo na kubatizwa kwa maji mengi bila malezi; haitoshi kumusaidia mukristo mpya kuwa na haki yake ya uridhi wa baraka na ahadi za Mungu zilizoko ndani ya Ibrahimu baba wa Imani (Wagalatiya 3:29; 4:1-2). Ndo maana Waefeso 6:4 inazungumuza kuhusu WAZAZI WALEZI ambao ni tofauti sana na wazazi wa kawaida yaani baba au mama aliye kuzaa kimwili. Hao wazazi walezi (mufano ya parain au marraine washauri kwenye ndoa) ni watu wamuhimu sana maishani mwetu na wana kazi kubwa sana, na moja wapo ni:
- Kumufundisha mtoto wao wa imani ili akomaye na discipline au nizamu yaani kumufundisha kuheshimu, kumutii Mungu kwa mambo yote na watu waliyo kutanguliya duniani au kwenye maisha yoyote (Waebrania 13:17);
- Kumuelekeza mtoto wao wa kiroho sawasawa na zawadi, karama, maono au mwito aliyo bebeshwa na Mungu ili asiende kwa kupapasa-papasa na kuingiya bila kutayarishwa vizuri kuhusu changamoto, upizani, matatizo yanayo mungoja huko mbeleni (Waefeso 4:11-12);...
- Kumutayarisha kusimama kama muzaliwa wa kwanza na ni vema atambuwe vita alivyo navyo kama mutangulizi katika imani (Weabrania 12:22-23); ili asije akakwamisha waliyo nyuma yake (kama yeye ni muzaliwa wa kwanza kwa cheo wala kwa haki au kama yeye amekuwa mtu wa kwanza kuokoka ndani ya jamaa yao) soma Warumi 11:16;
- Kuombea na kuimarisha imani yake ili isitindike anapopitiya majaribu mbali mbali hata apate kuimarika (Luka 22:31-32);...
Ø Kutoshika mambo yafuatayo inaweza pia kukwamisha maisha ya mkristo:
- Kuzarau na kushindwa kuheshimu vitu vitakatifu vya Mungu, kukataa kusikiya sauti, kushika na kutembea sawasawa na maagizo ya Mungu kwa kukataa maongozi ya Roho mtakatifu; ile tabiya inamufanya mtu aende inje ya
baraka za Mungu ingawaje; "Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?" Hesabu 23:19. Ndo maana Mungu kauliza Nabii Samueli : "Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema?" Sikiliza sasa: "Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu." (1
Samueli 2:29-33). "Naye Samweli akasema, je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu" (1
Samueli 15:22); Mungu ka sema na mufalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda: "Mimi nalisema nawe wakati wa kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu." (Yeremiya 22:21; 35:1-15); "Elisha akasema, Lisikieni neno la BWANA; BWANA asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula... Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao... Naye mfalme akamweka yule akida, ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia. " (2 Wafalme 7:1-2, 7, 17); "Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa BWANA; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese." (1 Mambo ya
Nyakati 10:13-14);
- Kushindwa kuvumiliya au kustahimili majaribu mbalimbali yanayo kuja kwako kama mutiyani ambao yana lenga kukuimarisha, kukupandisha ngazi wala sikukukwamisha (Yakobo 1:2-4, 12); ni vema sana kuwa na subira na kuondowa woga ili tusije tuka kwama kama wengine (1 Samueli 13:8-14);
- Kutoheshimu, kutoelewa mwito wala kutumikiya Mungu inje ya mapenzi yake kwa kujiingiza kazini bila kuitwa au kwa kuigaiga wengine waliyo fanikiwa kimaisha bila kujuwa ni kwa njia gani, nao wametoka wapi na Mungu, wana masharti gani au agano gani na Mungu wao,... Hapo mtu anakuwa muasi mbele za Mungu na inakuwa vigumu kufanikiwa inje ya agano na Mungu (Waefeso 4:11-12);
- Kutoa siri ya mwito wako au huduma kwa watu: mtu akisahau kwamba siyo kila kitu ndo anatakiwa kueleza mbele za watu, anaweza kwama; mufano wa ndugu Samsoni: Soma Waamuzi 13:5; 16:17-18; mfano wa mfalme Hezekiya soma 2 Wafalme 20:12-17. Nilazima kujuwa kulinda na kutunza siri ya Mungu ili ufanikiwe, soma Mika 7:5-6. Unaposoma habari za Yesu, utakuta kwamba alipo maliza kubatizwa na akashuhudiwa na Roho mtakatifu ya kwamba yeye ni mwana mpendwa wa Mungu, tena akaingiya hekaluni nakuchukuwa kitabu na kusoma unabii uliyo nenwa na Nabii Isaya kumuhusu; yaani mwito na kazi yake, vita vikamuinukiya na majaribu ya kazidi kuwa mengi, sababu siri imesha julikana (Luka 4:1-2, 18-19);
- Kuanza kazi mpya au huduma au tena kupandishwa cheo (position) bila kujali misingi iliyo tanguliya kwenye hicho kiti au position ya mpya ; ili mtu aanze kuishugulikiya mapema kupitiya maombi (Zaburi 11:3). Mfano ya Mufalme Daudi katika utawala wake kwenye kiti cha enzi katika Israeli; Israeli walipitiya njaa kali ya myaka 3; sababu ya zambi iliyokuweko kwenye kiti chake, wala si yeye aliye itenda. Aliyefanya thambi hiyo ni mufalme Sauli; mpaka Daudi alipoamuwa kumuuliza Bwana, ndo kapata suluhisho (2 Samueli 21:1-9).
N.B2: Mtu anapoendelea kumuomba Mungu ili ashugulikiye misingi mibaya, na Mungu anapo amuwa kuingiliya kati, haya ndio matokeyo :
- Kubomowa musingi (Ezekieli 30:1-4);
- Kufunuwa musingi (Mika 1:6; Ezekieli 13:14-15);
- Kuchoma musingi na kuiteketeza kwa moto (Maombolezo 4:11);
- Kutikisa musingi (Matendo ya mitume 16:26).
N.B3: Kisha Mungu
kuishugulikiya hiyo misingi ya uharibifu kumbuka, usisahau kumuomba tena ili aijenge kwa upya
kwa kutiya musingi uliyo bora na imara (Mathayo 7:22-27); sababu musingi
wa kiti cha enzi cha Mungu ni: Haki, Usawa, Fadhili na Uwaminifu; (Zaburi
89
:15). Na akitawala ni lazima mambo hayo yataonekana kwenye kiti au position uliyo nayo. Hapawezi kuwa upendeleo wowote, ukabila, ubaguzi wa dini, rangi, kikabila, kinjisiya... sababu Mungu, ni wa wote wenye mwili (Yeremiya 32:27); anaye nyesha nvua kwa wema na wabaya. Lazima watu wote wanufaike na hicho kiti (position au nafasi); sababu ni Mungu ndiye mutawala.
- Kiburi na majivuno au kujiinuwa mpaka mtu anasahau ya kwamba ni Mungu ndiye aliye muinuwa na kwamba anauwezo wa kushusha na kupandisha kila amupendaye; sababu Mungu anawapinga sana wenye kiburi (Yakobo 4:6b);
- Kukosa uwaminifu katika mambo yote zaidi mambo madogo (Luka 16:10-12); sababu ni lazima ku shukuruku Mungu kwa kila jambo (1Thes. 5:18);
- Kushirikiana na mtu ambaye maono yako hayaendi sambamba na yako: mwisho ni magogano, mabishano ijapo kuwa “pesa hazipendake fujo” wasemavyo watu wa mujini (Amosi 3:3; 2 Wakorintho 6:14-17; Mwanzo 13:14);
- Ni bora zaidi kuiombea Imani yako ili isije ikatindika unapopitiya majaribu mbalimbali; sababu Mungu anafurahiya kuwaona watoto wake wameimarika, kupitiya majaribu mbalimbali na wakisha kuimarika, waimarishe wengine pia kama baba au mama MULEZI na watangulizi au leaders (Luka 22:31-32); sababu imani ni kibebeo, ni kipimo au munzani ya capacity au possibility ya mtu; kwa hiyo Mungu hawezi kumupa mtu mambo au kumubebesha muzigo inayo muzidi uwezo wa kubeba. Mungu anataka mtu akomale, afunzwe na kuimarika kwanza, kabla ya kuzifikiliya baraka Zake (Warumi 12:3; Wagalatiya 4:1-2; 1 Wakorintho 10:13)
Ø Ni vema sana kuomba Mungu na kutafakari maneno yake usiku na mchana sababu:
- Usipo omba kwa bidii tena na imani, Mungu naye hawezi kukutendea kitu chochote (Luka 9:11c); na hali hiyo ni tangu bustani ya Edeni hapo Adamu na Eva walipo fanya dhambi, tangu siku ile; ili Mungu aingiliye ndani ya kesi zetu, inabidi kukuwe mtu ambaye aliomba kwa kumuonyesha haja ya mioyo yetu au ya mtu mwingine asimame kwa niaba yake mbele za Mungu (kazi ya Waombaji na Makuhani). Soma kitabu cha Wafilipi 4:6 na Yeremiya 33:3 vinaeleza waziwazi maneno hayo;
- Usipoweka imani yako ndani ya
maneno ya Mungu na yakawa ndani ya moyo wako, huwezi kamwe kufanikiwa au kujuwa la kuomba; maana ndani ya Biblia ndimo
munafichwa ahadi na siri zote za Mungu kwaajili ya kuwafanikisha wote waaminiyo Neno
lake; yaani Yesu Kristo (Yoshua 1:8; Yer 29:11-13); na ahadi
na baraka zote Mungu alizo muahidiya rafiki yake Ibrahimu baba yetu wa Imani na uzao wake
wote (Wagalatiya 3:29); Yesu mwenyewe alisema, mukiniamini, lolote mutakalo omba nitawapa (Yoana 14:12-15);
- Pasipo kuwa na maneno ya Mungu kwa uwingi, Huwezi kumushinda Shetani, ambaye bado anazunguka-zunguka kama simba angurumaye akimutafuta mtu amumeze soma (1 Petro 5:8-10) tena kumbuka kama Yesu alisema ya kwamba pepo muchafu atokapo mtu haendi mbali; kwa hiyo ni lazima kukesha sana, yaani kuwa mwangalifu ju ya thambi ambazo uliwayi kuanguka ndani; sababu ukirudi nyuma hali yako itakuwa mbaya zaidi kuliko ngisi ulivyo kuwa zamani, hilo ni neno la Mungu katika kitabu cha Mathayo 12:43-45;
- Neno la Mungu linataka, yaani kukutenga na zambi na kila kitu kisicho mupendeza wala kuheshimisha Mungu (Yoana 17:17) tena litakulinda ili usimutendeye Mungu thambi (Zaburi 119:11) yaani kumuasi Mungu kwa kuvunja sheria na amri zake (1 Yoana 3:4); tena Neno la Mungu pamoja na maombi ya imani iliyo imara ndani ya Kristo Yesu, ni moja wapo ya silaha za Mungu kwa kupambana na Mwovu Ibilisi pamoja na hila, ujanja na maarifa yake yote (Waefeso 6:18);
- Kuna pia Uzaifu kwa kumutumikiya Mungu na kutumiya karama au zawadi tulizopewa na Mungu (Yer. 48:10); na hii inatuma tusifikiye utimilifu na kuishi kiwango cha maisha Mungu alitaka tuishi hapa chini ya juwa;
- Uvivu kwa kufanya kazi sababu uvivu unaleta umasikini (Méthali
6:8). Mtume Paulo ka sema: “Asiye
tumika na asile” (2 Thes 3:10-12) na hiyo ni haki
sababu tangu shamba la Edeni, Mungu kasema na Adamu ya kwamba: “Mtu atakula kwa tabu au kwa jasho ya uso
wake”; (Mwanzo 3:19). Nilazima unapookoka kufanya kazi ya mikono kama umeitwa kuifanya; maana pana wengine wameitwa na Mungu kama Mtume Petro aliye achishwa uvuvi wa samaki, akawa muvuvi wa watu peke yake bila kusuka hema ka Mtume Paulo;
- Upuuzi au kuzarau; Upuuzi ni mubaya tena ni thambi mbele za Mungu (Yakobo 4:17); sababu hakuna ajuwae njia za Mungu wala wakati wake wa kumjiliya mwadamu (Isaya 55:8; Luka 19:41-44). Mfano, Ibrahimu angelizarau wale wageni na kuwachukuwa wa kawaida hangelipokea baraka ya mtoto wala kuibiwa siri kuhusu kuteketezwa kwa Sodoma na Gomora (Waebrania 13:2);
- Kutojuwa au Ujinga (Hose
4:6) na Kukatishwa tamaa (Hesabu
13:30-33); kumewapelekeya watu wengi wamulaumu Mungu. Kuelimika ni vema zaidi.
N.B4: Tusipo shika na kuzingatiya sana kwa makini mambo hayo na kuwa na nizamu (discipline) maishani; ni lazima tutaliya na kulalamika sana kama Ayubu mtu wa Mungu muchaji, mukamilifu na munyenyekevu; ijapokuwa tumemwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. (Ayubu 21:7-12). Kumbuka kwamba kuokaka, ni kwa neema tena ni kipawa cha Mungu kwetu, maana si kwa matendo yetu mema ili mtu asije akajisifu (Waefeso 2:8-9); lakini sasa inatubidi tuweke IMANI hiyo ndani ya Yesu Kristo kwenye matendo, kwa kuwa imani bila matendo imekufa, na hapo ndipo tutaweza valisha mwili ahadi za Mungu zilizoko kwa Ibrahimu baba yetu wa Imani (Yakobo 2:17-24; Marko 11:23-24; Wagalatiya 3:29).
Kwa mwisho, ni lazima ku ngangana na maombi ya TOBA kwa Mungu; ambayo lengo lake ni kusaidia mtu kubadilisha musimamo, mwenendo, matumizi (ya pesa na muda), mutazamo ya maisha, mawazo na tabia isiyo ambatana na mazigira ya sasa; ili uone vema opportunity zilizo mbele yako kwajili ya kukufanikisha kwenye eneo lako.
Utajuwaje kama tayari umeshatubu? Ni hapo, mtu anapo sikiya kuwa na ujasiri na amani ndani ya moyo wake, bila tena kujihukumu. Matendo ya Mitume 3:19-21 inasema: "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu." Na Wakolosai 3:15 "Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. Tena Wafilipi 4:7 inaongeza kusema: "Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu".
Ni lazima mtu atasikiya kuwa na amani moyoni mwake anapo chukuwa maamuzi ju ya kitu cha kufanya au jambo fulani. Usipo kuwa na amani au utulivu moyoni kisha kuchukuwa maamuzi au kupiga hatuwa; tambuwa kwamba hapo sasa ni Roho wa Mungu anakusemesha na anaendeleya kukudayi kufanya maombi ya TOBA.
Habari hizi Bwana wetu Yesu alizijuwa; sababu alipoanza kufundisha injili yake ya kwanza huku Kapernaumu; alianza kuwaambiya watu: "tubuni kwa kuwa ufalme wa mbinguni umekaribia". (Mathayo 4:17) Alijuwa wazi ya kwamba si vyepesi mtu ambaye hajabadilisha mutazamo wake wa ndani, musimamo, tabia, mawazo, mwenendo na hali yake ya zamani ni vigumu kuingiya kwenye ufalme mpya na kuendeleya bila shida.
Umenielewa? Ikiwa hujaelewa, tafadhali fuatana nami tena katika mfululizo mwingine wa somo hili, siku chache zijazo. Tuzidi kuombeana.
Ni mimi katika utumishi wa Kristo.
Pasteur Thaddée Bizy Barhazigirandi
UJUMBE WA NENO LA MUNGU KWA WATU WOTE
Umeletwa kwako na:
KANISA "MULIMA WA MAKIMBILIO"
Communauté des Eglises Evangéliques pour toutes les Nations-Unies
"C.E.E.N.U"
N° 005, Av. Mulungulungu, Quartier Panzi, Commune d'Ibanda, Ville de Bukavu-RD Congo
à moins de 100 mètres sur RN 2
Adresse mail : tbizyma@gmail.com, thaddemabize@yahoo.fr
Tél. : WhatsApp: (+243) 995416144: , +243 818216066.Facebook: Thaddée Barhazigirandi; Twitter: @ThaddeeBizimana
Linkedin: https://www.linkedin.com/in/thaddée-bizimana-b79301a8
.jpg)
Commentaires
Enregistrer un commentaire