RUDILIA UPENDO WAKO WA KWANZA MAANA HIZI NI NYAKATI ZA MWISHO USIJE UKAMALIZA MWENDO WAKO VIBAYA

 Usomi wa neno la Mungu:  

Ufunuo wa Yohana 2:1-7; Mathayo 24:3,9-12; Wimbo Ulio Bora 8:7

« Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu. » Ufunuo wa Yohana 2:1-7

 «Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. » Mathayo 24:3,9-12

« Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, Wala mito haiwezi kuuzamisha; Kama mtu angetoa badala ya upendo Mali yote ya nyumbani mwake, Angedharauliwa kabisa. » Wimbo Ulio Bora 8:7

I.   KIINGILIO 

Maana ya Upendo : sawa sawa na kitabu cha Wagalatia 5:22a « Upendo ni tunda la roho » ; yaani kitu cha rohoni na kwa kuitambuwa lazima pakuwe matendo mazuri. Kwa kuwa Yesu alisema : « tutawambuwa kwa matendo… » Ndo mana Mtume Yohana katuonya ya kwamba : « watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli » 1 Yohana 3:18. Kwa hiyo lazima kujuwa kwamba upendo ina vita vikali na vita vyake ni vya kiroho ; njo mana hatuwezi vishinda kwa kupigana kimwili. Kwa hiyo mtu akikuchukiya usikazane naye kimwili ; tafuta mbinu za kupatana naye tena kiroho kwanza kwa kutenganisha kilicho haribu uhusiano wenu bora wa hapo awali. Soma Waefeso 6:12.

 

II.    VIGEZO VYA KUONYESHA KAMA KWELI NDUGU MWENZAKO ANAKUPENDA

1 Wakoritho 13:4-8 « Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. »

Kwa kweli hatutagusiya vigezo vyote venye kutajwa ndani ya ile maandiko hapo juu; ila tu vile ambavyo tayari vimewekewa kistari chini yake.

Tufuate sasa vigezo au hali ya kuonyesha kama bado ndugu, rafiki, muke au mume wako ana kupenda kweli kweli na upendo halisi wa Agape ambao ndani yake hamuna kutafuta faida:

1.   Kuvumiliyana na kusaidiyana maana upendo huvumiliya yote : Kama kweli kuna upendo kati ya ndugu na ndugu watu watachukuliana mazaifu kama vile Yesu Kristo alivyo tuchukuliya makosa yetu vilevile ; akatufiya wakati bado tungali wenye dhambi : « Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. » Warumi 5:8. Amupendaye mwengine lazima atamuchukiliya uzaifu wake na kumuvumiliya wakati wa raha, tabu, upungufu au utajiri, ujana au uzee, afya bora au magonjwa, awe murefu au mufipi, munene au wa kugonda, mweusi au mweupe… Pasipo upendo wa Mungu na roho ya kuchukuliana mazaifu na kuvumiliyana kulingana na mila wala tabia ya kila kabila na taifa duniani, haiwezekani makabila, lugha na taifa kukaa ndani ya inchi moja kwa ushirika, pamoja hata kujenga jamii na taifa moja. Kama vile neno la Mungu linavyosema : « Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. » Matendo ya Mitume 17:26-28

Kwa hiyo sasa watu wengi, zaidi sana wakristo walio okoka kutoka dhambini; lazima kuvumiliana kama vile Yesu Kristo alivyo ambia mitume: «Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe. Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani. » Luka 17:3-5

2.    Hakuna cha kuoneyana wivu : anaye mupenda ndugu yake hawezi kumusikiliya au kumuoneya wivu kamwe; sababu wivu inapoingiya hapo ndo kwenye roho ya uharibifu nayo inapata nafasi na watu wana salitiyana, wanauwana kwa kupeyana sumu, kuendeyana ku waganga wa kyenyeji… na hapo upendo unapoa. Kama kwa kweli baraka za ndugu, jirani au rafiki yako ni kama baraka zako pia ; yaani mambo yote ni kwa ushirika ; sioni kwa nini roho ya wivu inaweza pata nafasi kati ya ndugu. Mungu wa mbinguni atusaidiye sababu hata kama ndugu yako haja kusaidiya kwa njia hii kuna siku utakuwa na lazima yake kwa njia nyingine kupitiya ile nafasi yake. Wivu na fitina vinaweza tuhombesha sana tena sana, na kurudisha nyuma maendeleo ya kanisa, jamaa, jamii na taifa ; sababu mtu wa wivu hawezi pongeza mwengine wala kupenda aendeleye mbele ; kuliko amupongeze anatamani kumuangusha ; ijapo ule mtu njo mwenye Mungu alifanya kuwa mutangulizi kwa kuwaangaziya wengine ili wamufuate. Kwa hiyo kuliko kuoneyana wivu, ni bora zaidi tuombeane kwa Mungu wa mbinuni ili Mungu aliye mukumbuka na kumuinuwa mwezetu nasi akatukumbuke na kutubariki pia.

Jameni wivu si kitu kizuri sababu maandiko matakatifu yalianza kutuonya zamani na kusema : « ….Upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu [Radi]. » Wimbo Ulio Bora 8:6

Mtu mwenye wivu mwenyewe anajifunga kuendeleya sababu kuliko aendeleye yeye, kazi yake kila siku, ni kufikiri namna ya kuangusha wengine waliomupita au walio mushinda. Mfano : Kwenye biashara au busness, kuliko wivu wa kutaka kulingana na kampuni jirani au muchuruzi mwenzako ambaye amekushinda soko ; lazima kubadili mbinu zako na mitindo kwa kuvutiya wateja kwa kufanya bora zaidi ya jirani zako; ndo inatwa marketing (masomo au elimu ya kuvifunza soko na mbinu za kuvutiya wateja kwa ajili ya byashara mbalimbali). Hata Mungu naye alimushauri Kaini na kumwambia : « BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. » Mwanzo 4:6-7

Kawaida hatutakiwi kuwa sawa maishani ; si lazima njia ndugu yako alipitiya nawewe ukazane mpaka tu uipitiye ; maana Mungu Baba wa mbingini ana njia nyingi za kubariki na anabariki watu wake kwa wakati wake mwenyewe. Mungu hana mushauri, anafanya alitakalo ; kwa hiyo acheni ile roho ya wivu ya baraka za wengine. Ombeni Mungu na kuwa nasubira maishaini pamoja na kumushukuru kwa ajili ya baraka za wengine walio barikiwa tayari na Bwana. Mtu anapofurahiya baraka za wengine ; Mungu naye anamufurahiya sababu hana wivu ndani mwake na ni lazima mtu yuho atabarikiwa pia. Kwa Mungu kuna kila kitu, kama ni ndoa nzuri yenye raha na amani, Mungu anao, kama ni watoto wazuri Mungu anao, kama ni pesa, utajiri, umaarufu ; nyumba, kazi na gari nzuri ; viza kwa wasafiri… Mungu Baba wa mbinguni ana kila kitu tena kwa utele na Yeye si muchoyo anapana bila upendeleo.

Mtu mwenye wivu ni tayari kumunungunikia Mungu ijapo manunguniko mbele za Mungu ni zambi ; ilituma taifa la Israeli wanakawia jangwani muda wa miaka 40; na waka umwa pia na nyoka za moto au sumu hata watu wengi kati yao wakafa huko jangwani (Hesabu 14:1-35 ; 21:5-6).

3.   Kufurahiyana yaani hakuna hasira wala uchungu moyoni: Kama kwa kweli mtu hawezi tena sikiya furaha wanapo kuwa pamoja ; ina mana upendo kati yao ulishaka zamani. Kama kwa kweli kati ya wanandoa hamuna tena furaha kati yao, ina maana pia upendo wao umepoa tayari; lazima sasa warudi haraka kwa Yesu ili wachocheye tena ile tunda la roho kabla adui hajajitukuza ndani ya ndoa yao; bila hivyo, lazima kutakuwa magonvi na matengano au kutokuaminiana tena hata kukaribisha roho ya uzinifu ndani ya ndoa yao kwa kwenda inje ya ndoa.

Kanisani, waliyo wengi siku hizi, kusalimiyana hawawezi tena, sababu ya uchungu moyoni ju ya mwengine ; na wakisalimiyana ni kwa unafiki. Hayo yote ni kizuwizo cha baraka ndani ya kanisa la Bwana, ndani ya huduma ya maombi… ; ndo maana waliyo wengi wanaomba na kufunga sana bila mafanikiyo au majibu ya maombi ; sababu Mungu wetu ni Upendo na wote huko mbinguni wanaishi kwa umoja na ushirika.

Tuombe ; Mungu Baba yetu wa mbinguni kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti ; atusaidiye kabisa, kuishi pamoja kwa furaha na amani; sababu watu wa wili hawezi kutembea pomoja pasipo kupatana na wakafikiye malengo yao. (Amosi 3:3).

4.Kuaminiana : watu ambao wanaaminiyana kukopeshana pesa kiwango chochote kile ; haiko shida kati yao na ile inaonyesha wazi kwamba wanapendana kabisa. Cha ajabu sasa nyakati za leo hata kati ya wakristo wa kanisa moja na ndugu walio toka ndani ya tumbo moja ; hiyo uaminifu hakuna tena kati yao. Na wakikopeshana wanawekeyana masharti mengi hata kulomba riba (faida ya zaidi 10-15 yaani unakopesha 10$ unarudisha 15$ haijalishi ni kwa saa moja) ; wala kartasi za nyumba, shamba, gari na vitu vingine vya samani ; ijapo neno la Mungu linasema : « Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida. Ikiwa wewe kwa njia yo yote wapokea nguo ya jirani yako rehani, lazima utamrudishia mbele ya jua kuchwa; maana hiyo nguo ni kifuniko chake, hiyo peke yake ni nguo ya ngozi yake; je! Atalalia nini? Itakuwa, hapo atakaponililia mimi, nitasikia; kwa kuwa mimi ni mwenye rehema. » Kutoka 22:25-27

Ni shida kwa watu wengi hizi nyakati kusaidia mtu yeyote wasiye mujuwa vema, sababu ya kuogopa huyo mtu atawaloga au kuwachawika na kuwafungia baraka zao kwa njia ya ushirikina. Na tunasikiya habari nyingi za kufanana hizo kwenye maombi ya ufungulivu. Hali hiyo imepunguza upendo wa ndugu, sababu hakuna uaminifu tena. Tuombe, Mungu Baba yetu wa mbinguni atuoneye huruma kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti.

5.    Kuwa na adabu : Kwenye upendo bado iko ni lazima watu waheshimiyane pia, watu hao hawawezi tetana wala kusengenyana inje, hakuna zarau, hawawezi ayibishana wala kuchambana mbele za watu na kukoseyana adabu hata kama kuna aliye koseya ; sababu atamuonya kwa upendo na upole na kiyasi pamoja na hekima za Mungu… Mfano : Kwenye ndoa Upendo ukipowa ndo hapo unasikiya mmoja anasema eti : « alikuwa anakojowa kitandani » na mambo mengine mengi ya ayibu mbele ya watu. Ijapo kuwa si halali kutangaza au kutowa siri ya kitandani au unyumba inje ; imeandikwa ya kwamba : « Ndoa na iheshimiwe na watu wote… » Waebrania 13:4

Sababu ya kukosa adabu kati ya watu, walio wengi wanafikiya kiwango ya kutukana na kuwapiga wazazi wao au viongozi wao na ile inaleta laana sana maishani na kupunguza pia miaka ya kuishi hapa duniani (Waefeso 6:1-3).

6.    Hakuna kujipendelea : Kwenye upendo iko, kila mtu hu tafuta kwanza faida ya mwengine mbele ya yote yaani kutaka kurizisha kwanza mwezako kabla ya kila kitu. « Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako » Wagalatia 5:14. Ndo wakati Yohana Mubatizaji alijibu na kusema « …Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu ; na mwenye vykula na afanye vivyo hivyo » Luka 3:11. Kwenye mila fulani kuna mithali inayo sema kama mwenye kumpenda mwezake « hata puja moja ya kalanga wanachangiya » sababu ya upendo. Shida ilioko leo ni sababu watu wote leo hawapendi kutosheka na vitu vya dunia, upendeleo imezidi sana na inapelekeya ukabila nayo inaingiya hata makanisani ; watu wanaulizana leo eti « ulitoka kijiji gani ? »; na wengine « je ni wa kwetu ule pia ? » kabla ya kumupanga kwenye hudumu fulani kanisani. Wapendwa hiyo haifayi kwenye kuko upendo wa ki Mungu « Agape ».

Watu wa siku za mwisho ni kama vile ile roho ya Kaini imewaingiliya tayari : « BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? » Mwanzo 4:9 Siku za leo hakuna anaye mujali tena ndugu yake ; kanisani wakristo wamoja wana vingi, vinavyo wazidi ; wanakula na kusanza wakati wengine wanalala jaa, na hakuna mwenye anajihukumu kwa hilo ; ndani ya muji jirani ya mtu hata angelala jaa haisumbuwi mtu yeyote eti tuko ndani ya muji kila mtu na maisha yake. Wapendwa wa Bwana, Mungu wa rehema atuhurumiye katika jina la Yesu Kristo kwa hiyo tabiya mbaya ; sababu ile ni roho ya Kaini abayo tumerizi bila kujuwa.

7.    Hakuna majivuno : Anaye mupenda mwingine hawezi enda anajitapa au kujivuna na kujieleza mbele ya watu sababu alimusaidia mufano na : chakula, nguo ya kuvaa, pesa… wala kumuombea akapona au kuokoka na hatari fulani. Siku hizi pana shida kwa wana ndoa zaidi sana wanapo pungukiwa na upendo kisha mtu moja kati yao ndani ya nyumba njo kafanikiwa kupata pesa au kazi, ndipo unasikiya eti « mimi njo byote, nilisha kuwa na muzigo ya kila kitu ndani ya hii nyumba… » Hali kama na ile inajitokeza mara na mara; sababu ya upendo kupowa. Kwa kweli yule ambaye anamupenda mwezake hawezi kamwe kumukumbusha kile kitu alicho mufanyiziya kama kweli aliifanya katika pendo. Mukristo akifikiya hiyo hali, hapo anaelekeya maanguko sababu hamurudishiye tena Mungu Baba wa mbingini sifa na heshima na utukufu ; anafikiri ni kwa nguvu, hakili wala uwezo wake njo maana ka fanyikiwa. Kwa mufano, Mwimbaji akijisifu eti yeye peke yake njo anajuwa kuimba na bila yeye wengine hawawezi imba vizuri kwa kumuimbiya Mungu ; pale wala hana hakili sababu mukono moja haiwezi piga ngoma, sababu akiimba bila wakumusaidia kuimba, wimbo wake hawezi koleya. Muhubiri naye akijivuna sababu mahubiri yake matamu, lazima akumbuke pia kama kuna wanao muchukuliya ndani ya maombi na bila uwepo wa Mungu hakuna mtu anaweza kusikiya yale mahubiri au kuokoka. Tukiwa na upendo ndani ya roho zetu hatuwezi kujisifu au kujivuna au kijitapa mbele ya watu. Sababu hiyo ni tabi aya watu wa siku za mwisho kama vile neno la Mungu linasema : « Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi. » 2 Timotheo 3:2

Mtume Paulo alituonya namna ya kujisifu nayo ni hii; « Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake. Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. » Wagalatia 6:3-5

8.    Hakuna hofu : Kwa kitabu cha 1 Yohana 4:18 neno la Mungu ninaeleza kwamba « Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo. » Mtu ambaye anamupenda mwengine hawezi muogopa kwa jambo lolote. Mfano : Unakutana mwanamke wa ndoa hawezi juwa lomba mume wake pesa za chakula sababu ya kumuogopa ; watu wakiwa ndani ya kundi moja (Kwaya, maombi, baraza la kanisa…) kisha wanaogopana wao kwa wao inamana hakuna tundu la Roho liitwalo upendo ndani ya hilo kundi. Shida hiyo inaonekana hata kwa wakristo : wanaogopa kuchangiya chakula eti wata wapa sumu ndani ya ile chakula au kuwanyanganya wala kuharibiya nyota zao kupitiya chakula; hata kwenye vikao vya baraza za makanisa kuchangiya ilisha kuwa shida sababu ya kuogopa sumu kwenye chakula na vinywaji. Nyakati hizi wakristo wengi wanaona ni heri kuchoma kwa moto mavazi yasio wastahili tena, kuliko kuipatiya ndugu mwenye anapungukiwa. Kuvaliana njo sitasema hata kama na haiko usirimu, tukiachana na mambo ya kiroho kumbuka pana magonjwa ya ngozi yenye kuambukiyana.

III.      KILICHO FANYA NIOGOPE SABABU YA KUKOSA UPENDO WA NDUGU

1.      Unapo mubariki adui yako pale pale unamulaani : sawasawa na neno la Mungu katika kitabu cha Warumi 12:19-20 « Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. » Warumi 12:19-20

Mfano : Mwalimu wa neno la Mungu Christopher Mwakasege, alikuwa karibu kumaliza mukutano wa neno la Mungu, akakusudiya sasa awabariki watu kama ilivyo desturi ; alipo inuwa mikono yake juu, akaona malaika wa Bwana anasimama na mupanga mikononi mwake, alipo uliza akaambiwa eti « ukiombea hawa watu baraka na ndani ya mukutano kuna watu ambao wanakusudiya kukumaliziya maisha, wao ndo wata kufa ; kwa hiyo waite ili uwaombeye rehema kwanza, » mwishowe akafanya kama alivyo ambiwa ; na kwa mushangao watu wawili wakaja kwanza pale mbele kwenye mukutano ya watu zaidi ya elfu kumi, akaangaliya akaona bado ule malaika angali anasimama akasema tena ndani ya mukutano kungali wengine ; kwa mwisho mwengine wa tatu akaja na waka shuhudiya makusudiyo yao ya kutaka kumaliziya Mwalimu Mwakasege maisha kwa sababu sisizo julikana. Na hapo, ule malaika akatoweka ndipo Mwalimu akawaombea rehema mbele za Bwana kisha sasa akaachiliya baraka ju ya mukutano wote bila shida.

Haiko ungwana watu wasio shirikiana, kupatana, kusikilizana, watu ambao wako na mizozo ambayo haija tatuliwa kuchangiya chakula au kinywaji. Kumbuka shida iliyo mupata Yoshua na wana Waisraeli walipo chukuwa chakula (mikate) na divai ya watu wa Gibeoni (Wahivi) na kutumiya kisha wakafanya nao agano kumbe ni kwa ujanja (soma Yoshua 9:1-27).

Shida ni sababu wakristo wengi wanachangiya chackula cha Bwana yaani meza matakatifu pasipo kupatana wala kupendana ; kumbe hapo kuna laana ambazo zinaweza kuwapata watu wasipo kengeuka na kuanza mbele ya kutumiya kulombana musamaha kabla ya kula meza matakatifu ya Bwana. Sababu Yesu alisema hivi kuhusu sadaka : « Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. » Mathayo 5:23-24. Tena ikumbukwe kwamba hicho ni chakula cha ushirika, halama ya kuonyesha kama tuko ushirika na tunashiriki pia mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo sasa mpaka atapo rudi kuchukuwa kanisa lake; yaani tunafanya kwa ukumbusho sawasawa na maagizo yake.

 

2.  Unapo tumikia Mungu bila Upendo unafanya kazi bure : Sawasawa na Neno la Bwana « Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. » 1 Wakorintho 13:1-3

Watu kama na hao ndo watakuja mbele za Mungu siku ya mwisho kisha Bwana atawafukuza kwa sababu neno la Mungu ninasema: « Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. » Mathayo 7:21-23

3.   Bila upendo kwa ndugu yako unaye mwona, Mungu anakuandikiya dhambi ya uwongo : « … Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. » 1 Yohana 4:19-20. Bila kusahau kama waongo wote ni katika lile ziwa la moto; soma kitabu cha Ufunuo wa Yahana 20:8;

4.    Unapo kosa upendo kwa ndugu yako, unaitwa mwuaji mbele za Mungu : Sawasawa na Neno la Mungu : « Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji : nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele » 1 Yohana 3:15. Hata kwa kitabu cha Mathayo 5:21-22 ; inaeleza pia kwamba mtu huyu anastahili hukumu : « Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. »

Woga yangu ni kuona wapendwa wengi leo wana kaa na chuki kati yao ; kisha siku moja mbele za Mungu akufukuze na kujikuta pamoja na wauaji wa kubwa zaidi kama wale wauaji wa Beni na Ituri inchini DR Congo na mahala pengine duniani wanao waua ndugu zao kwa kuwachiza na kukata singo bila huruma. Itakuwa ole sana, kwa hiyo watu lazima kufanya angalisho sana.

 

5.     Bila upendo Mungu hawezi kaa ndani yetu : neno la Mungu linasema : « Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu. » 1 Yohana 4:11-12. Kumbe ile kukosa upendo ndo sababu ya Roho wa Mungu kutosikika tena na kusema na kanisa ndani ya mikutano ya watakatifu walio wengi leo, sababu Mungu hakae tena ndani yao na wana kusanyika si kwa kusudi la Bwana bali kwa kusudi lao wenyewe.

 

6.   Pasipo kuwapenda kwa kuwasaidia wanyonge na kuwahurumiya wasiojiweza : mayatima, wajane, wamaskini, wakimbizi au wahamiyaji na wafungwa gerezani,… twafanya kazi bure mbele za Mungu kama kanisa: sababu: « Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa. » Yakobo 1:27 Itakuwa vigumu kupata baraka za Mungu hata tungeliomba sana na kufunga. Bwana Mungu ka sema na wana Waisraeli kupitiya Musa : « Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini; lakini mfumbulie mkono wako kwa kweli, umkopeshe kwa kweli yatoshayo haja yake katika ahitajiayo. Jitunze, msiwe na neno lisilofaa moyoni mwako, kusema, Umekaribia mwaka wa saba, mwaka wa maachilio; jicho lako likawa ovu juu ya nduguyo usimpe kitu; naye akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako. Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako. » Kumbukumbu la Torati 15:7-11

 

IV.      KWA KUMALIZA :

Nimegunduwa ya kwamba kinacho tuma watu hawapendane tena ndani ya ndoa, kanisa, taifa, jamaa na jamii si kingine ni roho za masheteni au udanganifu ambazo zinawaonyesha wamoja wetu kwamba wao ni tafauti (spécial) na wengine ijapo kuwa neno la Mungu linatukumbusha kwamba tuliumbwa sote kwa mufano wa Mungu, tena tunaye baba moja yaani sote tuko « wana wa Adamu » ama « wanadamu », ndugu yako ajapo kuwa mume au mwanamke sote tuko na baba moja sababu neno la Mungu ni kwamba: « Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa. » Mwanzo 5:1-2

Utofauti wa njisia au gender, lugha, kabila, rangi, kimo, muonekano wowote wa inje, utajiri au umaskini; hayo yote yasingelikuwa kikwazo kwa wanadamu maana sote tulitoka ndani ya mtu moja kama tulivyo isoma pia kwa kitabu cha Matendo ya mitume 17:26-28 « Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake. »

Sikitiko kubwa ni sababu ile roho ya kimapepo imesha ingiliya pia kanisa, mwili wa Kristo mpaka matengano, chuki, zarau, mauaji, ukabila, wivu wa cheo, kusalitiana, kusengenyana, kubaguwana eti huyu siyo wa kwetu, kutengana bila sababu, uchoyo, kujipendeleya (kupenda pesa kuliko Mungu), na kazalika. Nimegunduwa ya kwamba neno la Mungu liko wazi, sababu mahali ambapo Roho ya Mungu haiko tena ni roho ya Shetani ndo inatawala otomatikali; sababu pana matunda ya roho na matunda ya mwili; ivi watu wa Mungu hawapendi tena uongozi wa Roho mutakatifu, ni vigumu sana kutoa pia matunda ya Roho ambayo: «…ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi;... » Wagalatia 5:22-23 

Ukitazama hiyo matunda ndani ya jamaa zilizo nyingi nyakati hizi hamna tena, kwanza utakutana kama ni vigumu sana mukubwa na mudogo wachangiye tena au waikale kikao ambacho sicho cha kusamba au kutatuwa mizozo kati yao; kukaa pamoja kwa umoja wazungumuze na kuomba Mungu wakiimba kwa zaburi za sifa ; ni vigumu sana. Kwa sababu watu walimukaribisha Shetani pasipo kujuwa au kwa kujuwa kupitiya hirizi au uchawi, kushiriki ibada za sanamu na kupiga ramuli.

Ukitazama ndani ya Baraza nyingi za makanisa za Kikristo nyakati hizi utakutana hayo matunda hamna tena sababu wengi wao hawataki tena uongozi wa Roho mutakatifu ; na njo mana kuliko kutowa matunda ya Roho wanaanza kutowa matunda ya mwili ambayo ni : «…uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. » Wagalatia 5:19-21

Shinda ingine ni kuona kanisa ambalo ni bibi arusi wa Kristo Yesu, wenyeji wa mbinguni, ambalo lina kazi kubwa ya kuandaa bibi arusi ili kumulaki Bwana arusi siku ya mwisho, na wana ahadi hiyo na taarifa ya kwamba siku za mwisho zimekaribia ; (sababu dalili zote ziko wazi) ; nalo limelala na kuanza kuiga dunia. Ndo maana Roho wa Mungu iko analiya sana kwa ajili ya bibi arusi. Kwa hiyo, itakuwa ole sana kama parapanda litaliya na bado bibi arusi haja toka ndani ya usingisi na machafuko ya kila aina ambayo amejikokotea.

Ujumbe huu ni kwa ajili ya kuamsha tena kanisa la Bwana na jamii yote na kuwakumbusha ili turudiliye upendo wetu wa kwanza ; asije Baba yetu wa mbinguni kunyakuwa kinara chake ju yetu kama vile neno lake linavyo eleza katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana 2:1-7 « …Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu… »

Kanisa la Mungu, fanyeni angalisho, amkeni na kutoka katikati yao ; musije muka maliza kwa mwili kama alivyo liya Mutume Paulo kwa kanisa la Wagalatia eti : « Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani? Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli. » Wagalatia 3:1-4

Kanisa la Bwana amkeni tena kwa maombi na kukesha ili kufukuza hii ulozi aliyo uona mutume Paulo kwa kanisa la Wagalatia. Sababu imeonekana hata leo kwamba adui hajabadilisha mbinu zake, anatumiya ulozi kwa kuwatenganisha wakristo kati yao makanisani ili wasiendeleye mbele katika roho ; na hapo Yesu atakapo rudi awakutane wakigombaniya vyeo makanisani pamoja na chuki na mauaji kati yao ; wakitafuta sifa za wanaadamu kuliko kutafuta majina yao yaandikwe kwenye kitabu cha uzima.

Mungu Baba yetu wa mbinguni alioneye huruma tena kanisa lake sababu limeingiliwa sana na hii roho ya ulozi au uchawi. Mungu iliye Bwana wa kanisa alisaidiye kanisa lake lipokeye hii mashauri ili lipate kupona, lirudi tena kwenye misingi ya mitume na manabii (Waefeso 2:20-22) na kurudiliya upendo wake wa kwanza.

Kwa mwisho neno la Mungu linamalizia kwa kusema : « Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. » Warumi 13:8-10

N.B : Kumbuka Yesu yu waja upesi kumulipa kila mtu sawasawa na matendo yake usije ukakosa kuingia mbinguni kwenye raha ya milele sababu ya matendo na tabiya yako mabaya ya kukosa upendo.


Umenielewa? Ikiwa hujaelewa, tafadhali fuatana nami tena katika mfululizo mwingine wa somo hili, siku chache zijazo. Tuzidi kuombeana.

Ni mimi katika utumishi wa Kristo.

Pasteur Thaddée Bizy Barhazigirandi

UJUMBE WA NENO LA MUNGU KWA WATU WOTE
Umeletwa kwako na: 

KANISA "MULIMA WA MAKIMBILIO" 

Communauté des Eglises Evangéliques pour toutes les Nations-Unies

                                      "CEENU"

N° 005, Av. Mulungulungu, Quartier Panzi, Commune of Ibanda, Jiji la Bukavu-DR Congo; chini ya mita 100 kwenye RN2

Barua pepe: tbizyma@gmail.com, thaddemabize@yahoo.fr 

Simu. : WhatsApp: (+243) 995416144, +243 818216066.

Facebook: Thaddée Barhazigarndi; 
Twitter: @ThaddeeBizimana
Linkedin: https://www.linkedin.com/in/thaddée-bizimana-b79301a8

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

KWA NINI MTU MWENYE THAMBI ANAPO AMINI YESU KRISTO, KIPATO CHAKE NI KAMA KINA ZOROTA?

RETOURNEZ VOTRE PREMIER AMOUR CAR NOUS SOMMES AUX DERNIERS JOURS, AFIN DE FINIR VORE COURSE AVEC SUCCES

LE PECHE ET SES CONSEQUENCES DANS NOTRE VIE: