NYAKATI AMBAZO MUNGU ALIWEKA CHINI YA JUA

USOMI : Muhubiri 3:1-8; 9:11-12

Kwa kumutumikiya Mungu vizuri, ni lazima sana kuzifahamu nyakati hizi (tatu) ambazo Mungu alizitenga na kuziweka chini ya juwa; sababu ni lazima zijitokeze kwa kila mtu au mkristo wa kweli kuzishi.

Nyakati hizo nazo ni hizi zifuatazo: 

1) WAKATI WA SHIDA AU MATATIZO (KIPINDI CHA KUSHUKA): 

Wakati huu mambo fulanifulani yanajitokeza nayo ni: Magonjwa; kusingiziwa mambo usiyo ya juwa, kukosa kibali na samani mbele za watu, kufukuzwa nyumbani kwa wapangayi, mavalio zaifu au yenye kuchakaa, kukula kwa shida, kuomba msaada kwa ndugu na rafiki bila mafanikio, kukosa kazi, biashara kuhomba, kuibiwa, kuonelewa, kuchekelewa, ... (Mfano hai: (Ayubu kwa sura ya kwanza mpaka sura ya 37; Nabii Eliya nyakati za Yezebeli, Yesu Kristo musalabani, na kila mtumishi wa kweli lazima ahonje hicho kipindi.)

N.B.1: Wakati huu: Ni lazima mkristo ajuwe kuvumilia mateso, kuacha mihali na lawama na kubaki mwaminifu mbele za Mungu bila kupunguza neno; yaani kuwa na musimamo na Imani katika Kristo Yesu. (Soma 1 Petro 2:19, 23; 2 Samueli 24:10-16).

 

2) WAKATI WA KUTOWEZEKANA (KIPINDI CHA TAMBARARE): 

 

(soma Zaburi 31:13-15): Wakati huu ni tofauti kidogo na wakati wa mbele; sababu mtu haiko tena mukosefu wasana: chakula anaweza kupata, majaribu yanaanza punguwa kidogokidogo,... Hata hivyo, bado mtu ni muhitaji maana hajatosheka vilivyo kwa kile alicho nacho. Sababu akikula, ni kama kutuliza tu njaa kama ilivyo onekana kwa wakati wa kipindi cha kwanza. Akivaa nguo ya mpya ni marahaba au labda alipewa, ana niya ya kupana ila hana ya zaidi; maana yeye mwenyewe haitosheleyi kwa kujibu mahitaji yake (ingawaje mwanadamu hawezi kutosheka). Kwa wakati huu kuna hali ya vifungo na vipingamizi ndani ya kila kitu :

  • Maombi: mtu anaomba ila nikama maombi yake yanagonga mwamba na hayaendi fasi, ni kama yana murudilia;
  • Kazi: Mshahara hakuna;
  • Marafiki hukimbia: hakuna wakukujali, sababu wao ni matajiri na hakuna ushirika kati ya tajiri na maskini sababu wana tengana kimawazo;
  • Kila kitu kina kwama: kama ni miradi haiendeki, kama ni biashara wapi, mifugo na shamba haviendeki, mtu ana kopesha hakuna wakumukopa; sababu wanadamu hu musaidia mtu kwaajili ya faida;
  • Hali yake mtu huyo ni kama hakuna anaye ijali, wala kumuonea huruma: watu wote wana kusahau, sababu Mungu naye ni kama vile amekusahau au kukuacha. Na asipo kukumbuka, hakuna awezaye kukumbuka pia. (ila kumbuka Mungu hawezi kukuacha Yeremi 23:23; Isaya 49:15-16)

N.B.2: Wakati huu:

  • Walio wengi huanguka na kumuacha Mungu na kwenda kutafuta msaada kwa wanadamu na miungu (isio weza kusaidia wala kuokowa sawa na neno la Mungu kwa Zaburi 115:4-8); (1 Samweli 28:6-20)
  • Maswali na mawazo, mara yana kuwa mengi (hata mtu anafikilia kuanza kutubu na kutengeneza zambi asiyo zijuwa wala kuitenda; alakini kwa kweli maombi yao ni ya lazima sana kwaajili ya kuomba musahada wa Mungu);
  • Maneno yana kuwa mengi sana (hata kukiri mazaifu na kuomba vibaya. Mfano Esau (Mwanzo 25:29-33). Ila ni lazima kuomba Mungu hekima ili auzuwiye ulimi wako usinene mabaya. (1 Petro 3:10)

Bahati iliyoko, katika nyakati hizo mbili za mbele, Mungu humufichia mtu wake aibu, kwa ngisi kama mtu mwenyewe hakujieleza mbele za watu, hakuna awezaye kutambuwa kinacho endelea. Na tujuwe kwamba si vema zaidi, mkristo kujielezaeleza mbele ya wapagani, sababu, ile kujieleza mbele ya wasioamini inashusha heshima ya Mungu, tena mtu anaweza kujitoa mbele za maadui. Wakati mwengine kimya ni silaha ya kutisha adui; sababu kwa kweli adui wa mtu, hawezi kujuwa kilichoko moyoni mwako pasipo kupewa taarifa; ndo sababu utasikia adui akisema eti “ule hakosaki kitu ni boss au anakujia eti unikopeshe pesa kidogo” ijapo kuwa unaumiya sana na ukosefu. Hata ungelikusudiya kufanya kazi ya wabeba mizigo au ya kuzarauliwa; lakini watu watakukimbia na hakuna wakukupa kazi sababu hali yako na ya wafanyakazi ya kuzaraulika munatofautiana sana; yaani mtu huyo ana utukufu wa Mungu.

N.B.3: Ikumbukwe ya kuwa nyakati hizo mbili za mbele ni nyakati za ukimya kati ya mwanadamu na Mungu watu wengi wanafikiri (sababu ya kutozijuwa vizuri); kwamba Mungu amewaacha, amekwenda mbali nao, Mungu hawasikii, Hawaoni, au eti Hawapendi…,) kama ilivyo tukiya kwa ndugu AYUBU.

Tangu mwanzo ya mateso yake (Ayubu sura 1 hadi sura ya 37) Mungu akawa kama vile hamuoni wala hamusikii, (lakini tukichunguza maandiko vizuri, utakuta kama “Mungu ni Mungu aliye karibu nasi” soma (Yeremia 23:23; Mt. 17:27), tena yeye ndiye (NIKO AMBAYE NIKO) soma (Kutoka 3:14).

Hapo Ayubu akawa na maneno mengi tena mazito, asiyo ya chunguza mbele ya kuyatamka, hata akaanza kuzilaani siku zake za kuzaliwa na mtu aliye leta habari ya kwamba kumezaliwa mototo mwanaume. Lakini mara, hapo Mungu alipo mujiya, kunako sura ya 38-41 ya kitabu cha AYUBU; kaanza kujutia, alipo shindwa kumjibu Mungu, kwa maswali mazito, Alio muuliza. Ikambidi Ayubu, akiri na kutubu mbele za MUNGU, akaomba musamaha. Soma (Ayubu 42:1-6).

N.B.4: Katika nyakati hizo mbili, ni lazima kila mtu apime na kuchunguza sana masemi yake, ili asije akakiri mazaifu au kuomba vibaya; sababu Mungu anasikia mambo yetu yote; hata kama hatajibu papo hapo, sawa sawa na ngisi tulivyo omba. Soma (Matayo 12:36-37 na Muhubiri 12:14).

N.B.5: Wakati huo mwanadamu, ni lazima aombe Mungu, na kuacha kulalamika au mwenye kulaumu: Mungu, watawala au viongozi na watu wengine. Sababu ndani ya kulalamika kuna kukata tamaa, kupoteza tumaini na kupungukiwa Imani. Lakini katika kuomba mwanadamu anaonyesha hitaji kwa Imani aliyo nayo katika uweza wa Mungu kumusaidia matatizo au majaribu yalioko. Ni bora Zaidi kuacha kumunungunikia Mungu, sababu manunguniko na malalamiko, hayawezi kumaliza taabu hiyo wala kubadilisha hali yo yote ile. Lakini, kila mtu aelewe ya kwamba ni WAKATI, tena itapita, sababu hakuna linalo dumu hapa chini ya jua (soma Habakuki 1:2-3). Ukisoma vizuri mwanzo ya kitabu cha Nabii Habakuki, utagunduwa kwamba alibaki muda mrefu akilaumu kila mtu: watawala, hata na Mungu pia sababu ya kutomujibu: Ee BWANA, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia sababu ya udhalimu, ila hautaki kuokoa!” (Soma: Habakuki 1:2-4). Wakati huo, Nabii Habakuki akasahau kuomba Mungu, kafikiri kulalamika na kulaumu kwake kunaweza leta suluhisho kwa tatizo lake na la taifa lake.

Ingawaje yeye kuwa Nabii wa Mungu, lakini Mungu akamunyamaza mpaka kwenye sura ya pili, hapo sasa Habakuki kaanza maombi, nakusema: “Mimi mitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na njisi nitakavyojibu katika kulalamika kwangu”. Ndipo Mungu naye akamujibu akisema: “...Mwenye haki wangu ataishi kwa Imani yake”. Soma (Habakuki 2:4b).

 

3)  WAKATI  WA UTUKUFU WA MUNGU (KUINULIWA WALA KUPANDISHWA NGAZI). (YOHANA 11:38-44; 1 WAFALME  18:36-40)

Wakati huu, kila kitu kinaendeka vizuri: mahitaji yanajibiwa, kazi zinafunguka, jamaa inaongezeka, Amani katika unyumba, marafiki wanakuja wengi, majaribu yanapunguwa.

N.B.1: Kwa mtu mwenye kuwa katika hicho kipindi, kufanikiwa kwake hakuombi tena maombi mengi ya mafungo; wala kuhangaika kwa kwenda huku na kuku akitafuta msaada ya maombi. Utukufu wa Mungu ukiweko, ni lazima Baraka nazo zitajitokeza bila shaka. Sababu, Baraka za kiroho huwa zinakokota kama asimaku Baraka za mwili au mafanikiyo.

N.B.2: Hapo ndipo watu wengi, kati ya wasioamini uwezo wa Mungu, husema kwamba: “mtu huyu alienda kuzimu”. Wakati wa utukufu, ni wakati wa furaha, raha, salama, na amani, upendo. (lakini ni lazima kukumbuka neno hili : “...Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu asema BWANA wa majeshi”. Zekaria 4:6. Soma pia Isaya 48:3-11; Kumb. 9:5-7. Il mwanadamu asije akajiinula au kujikweza na kutawaliwa na kiburi wala majivuno nataka kugusa wala kuuchezeya utukufu wa Mungu).

ANGALISHO WA PENDWA: Fahamuni ya kuwa, nyakati hizo zote, ni Mungu ndiye aliye ziweka, na ndiye anaye ziruhusu; soma (Muhubiri 3:1-8); ili atukuzwe, na kuangalia uaminifu wako mwanadamu (soma Kumbukumbu 8:3-6, 15-19). Sababu kunakuwa “wakristo wa nyakati za utukufu wa Mungu au Raha na Amani pekee yake, wasio vumiliya kupitishwa jangwani”. Lakini si hivyo, sababu Mungu anataka tuwe wakristo wa nyakati zote (Mwimbaji wa nyimbo za Wokovu n° 131; anaimba akituhimiza eti: “Mimi mkristo nita'vyokuwa katika yote mpaka kufa. Mimi mkristo, 'navyoshuhudu, dunia yote ikinicheka... Mkristo katika kila hali, na nikiitwa na kufa tena, kwa raha kubwa nitakubali kuchukuliwa mbinguni juu.” Ukumbuke ya kwamba, usipo tembea kwa uaminifu katika nyakati hizo zote, unaweza kupoteza zawabu au taji ya ushindi ambayo Mungu aliwekea kila mushindi, mwadamu akishindwa kuvumiliya na kustahimili; itakuwa ole sana kwake! Soma (Yakobo 1:12).

 

Umenielewa? Ikiwa hujaelewa, tafadhali fuatana nami tena katika mfululizo mwingine wa somo hili, siku chache zijazo. Tuzidi kuombeana.

Ni mimi katika utumishi wa Kristo.

 Pasteur Thaddée Bizy Barhazigirandi

UJUMBE WA NENO LA MUNGU KWA WATU WOTE
Umeletwa kwako na:

KANISA "MULIMA WA MAKIMBILIO" 

Communauté des Eglises Evangéliques pour toutes les Nations-Unies

                                      "C.E.E.N.U"

N° 005, Av. Mulungulungu, Quartier Panzi, Commune d'Ibanda, Ville de Bukavu-RD Congo

à moins de 100 mètres sur RN 2

Adresse mail : tbizyma@gmail.com, thaddemabize@yahoo.fr 

Tél. : WhatsApp: (+243) 995416144: ,  +243 818216066.
Facebook: Thaddée Barhazigirandi; Twitter: @ThaddeeBizimana
Linkedin: https://www.linkedin.com/in/thaddée-bizimana-b79301a8

 

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

KWA NINI MTU MWENYE THAMBI ANAPO AMINI YESU KRISTO, KIPATO CHAKE NI KAMA KINA ZOROTA?

RETOURNEZ VOTRE PREMIER AMOUR CAR NOUS SOMMES AUX DERNIERS JOURS, AFIN DE FINIR VORE COURSE AVEC SUCCES

LE PECHE ET SES CONSEQUENCES DANS NOTRE VIE: