MAANA YA MACHOZI YA MUKRISTO MBELE ZA MUNGU WA MIUNGU

USOMI : Waebrania 5:7 ; Yohana 11:35 ; Zaburi 126:5 ; Ufunuo 7:17

Kwa Utangulizi wa hili somo; kwanza nianze kukupa tahazari ; sababu kila mtu ana mutazamo wake wa kipeke (interpretation) kuhusu kuliya au kutoa machozi mbele za Mungu sababu ya jambo fulani fulani isiyo kuwa ya kawaida maishani mwake :

1. Machozi kwenye maombi mbele za Mungu kamwe haitokani na mtu binafsi; kwa hiyo  si vema kulazimisha mtu kuliya au kumunyamazisha anapoliya mbele za Mungu kama hakuna uongozi wa Roho wa Mungu ; sababu hatujuwi kuomba ndivyo neno la Mungu linasema katika kitabu cha Warumi 8:26-27 : « Kadhalika, naye Roho anatusaidia katika udhaifu wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni [kuuguwa] usioelezeka. Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya watu, anajua fikira ya huyo Roho; kwani huyo Roho huwaombea watu wa Mungu kufuatana na mapenzi ya Mungu » ;

 

2.  Alakini pia siyo kila kilio au machozi ni halali au inatakiwa mbele za Mungu ; sababu pana machozi mengine Bwana alikataa kusikiliza hata mengine inaleta hasara mbaya kwa mwili wetu binafsi. Mfano :

a. Machozi iliyo kataliwa mbele za Mungu:

-   Esau aliliya mbele za Mungu kisha kukoseya kwa kutowa haki yake ya Uridhi; ila hakukubaliwa mara tena sababu, hakutubu kwanza; soma katika kitabu cha (Waebrania 12 :17) ;

-       Taifa la Israeli lililo toka inchini Misri ; lilishindwa kuingiya Kanani, kwenye inchi ya ahadi, (isipo kuwa Kalebu na Yoshua); sababu wengine waliliya mbele za Mungu, sababu ya hofu ya adui na kuwanungunikiya watumishi wa Mungu (Musa na Haruni); wakashusha heshima ya Mungu aliye waongoza na kuwatoa inchini Misri; kwa kutomuamina na kumutegemeya, kwamba anaweza hata kuwaokoa na mikono ya Wanefili (Hesabu 14:1-3, 11-12);

-     Nehemia pamoja na Kuhani Ezra na Walawi, walizuwiya kwa kuonya wana Waisraeli wasiliye machozi mbele za Mungu; sababu furaha ya Mungu ndio nguvu zetu. (Nehemia 8:9-12);

-   Nabii Yeremia alipo sikiya wana Waisraeli wakiliya machozi sababu ya uchumi kuharibika na kukosa Amani; Mungu akamusemesha na kuwaambiya ya kwamba wazuwiye sauti zao, wasiliye kwa machozi, na macho yao isitoke machozi; (Yeremia 31:16);

-       Yesu Kristo katika safari ya kwenda Golgotha alikataza wanawake walio kuwa wakiomboleza na kumulilia akisema: ...Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu. (Luka 23:27-28);

 

b. Mazara au hasara mbaya ya kutoka machozi:

-     Mtumishi wa Mungu Ayubu alijikuta uso wake umeharibika na giza likaingiya katika kope zake sababu ya machozi (Ayubu 16:16);

-     Mufalme Daudi naye vilevile alijikuta jicho lake limeharibika na kuchakaa kwa sababu ya machozi mengi ya kila usiku kitandani mwake, hapo adui zake walipo muinukiya (Zaburi 6:6-7);

N.B: Zaidi ya hayo, machozi ya aini hii ya Mufalme Daudi, yana maanisha ya kwamba nafsi ya mtu wa namna hii, imeumiya sana na hajapata uponyaji wa jaraha lake; maana nafsi inapo choka kubeba uchungu lazima isukume kwenye mwili; maana hatutakiwi kubeba hasira yenye uchungu zaidi ya masaa kumi na mbili (12h00), sawa sawa na neno la Mungu: “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.” (Waefeso 4:26-27).

 

3.Angalisho: usi muchokoze kwa kumulilisha machozi ; mtu ambaye anapendwa sana na BWANA Mungu. Mfano watumishi wa Mungu, mayatima na wajane, wanyonge, …

· Mfalme Daudi katika vita vyake alimuliliya BWANA Mungu katika maombi na kusema: Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakieleza kitanda changu; Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu. Jicho langu limeharibika kwa masumbufu, Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi. Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu; Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu. BWANA ameisikia dua yangu; BWANA atayatakabali maombi yangu. Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, Watarudi nyuma, kwa ghafula wataaibika. (Zaburi 6:6-10). Tena Mungu anasema hivi:“Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.” (Zaburi 12:5)

·   Mtu wa Mungu anapoliya na kutosha machozi kwenye mazabahu ambayo inakubaliwa na Bwana, Mungu hafurahi sawasawa na andiko hili : Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia. (Malaki 2:13)

  Lakini pia mtu wa Mungu lazima atambuwe ya kwamba yeye analinganishwa mbele za Mungu sawasawa na mzazi mulezi; ambaye hasitahili kumuchokoza mtoto; vile vile, mukristo naye ni lazima asimame au kukaa kwa nafasi sawasawa na mtoto ndani ya jamaa; ambaye anatakiwa kuwaheshimu na kuwatii wazazi wake (Mtumishi wa Mungu); sawasawa na neno la Mungu: Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.” (Waefeso 6:1-4).

 

4. Siyo kila kuliya machozi, inamaanisha kwamba mtu ni zaifu; sababu machozi inabeba ujumbe mbalibali au tofauti na ni Roho wa Bwana tu njo ana uwezo ya kutofautisha na kutafsiri lugha ya kila chozi mbele za Mungu. Mfano:

 

* Kuna kuliya machozi sababu ya Upendo: Yesu alipofika kwenye kaburi ya rafiki yake Lazaro aliliya, (Yesu akalia machozi. Basi, Wayahudi wakasema, "Tazameni jinsi alivyompenda!") (Yohana 11:35-36). Hata Mtume Paulo naye aliandika : “Nilipowaandikia hapo awali katika hali ya huzuni na sikitiko moyoni na kwa machozi mengi, haikuwa kwa ajili ya kuwahuzunisha ninyi, bali kwa ajili ya kuwaonyesheni kwamba nawapenda mno”. (2 Wakorintho 2:4);

 

*   Mtume Paulo alitumiya machozi muda wa miaka tatu kwa kuonya : “Kwa hiyo, muwe macho mkikumbuka kwamba kwa muda wa miaka mitatu, usiku na mchana, sikuchoka kumwonya kila mmoja wenu kwa machozi”. (Matendo ya Mitume 20:31);


* Kuna kilio yenye kudayi haki au maombi ya kulipiza kisasi: Yesu mwenyewe alitowa mufano wa mama mujane aliye zulumiwa kwa kunyimwa haki yake na Hakimu; kisha Bwana yesu anauliza : “Je, ndio kusema Mungu hatawatetea wale aliowachagua, ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasikiliza? Nawaambieni atawatetea upesi.” (Luka 18:7-8a); Mtumishi Ayubu katika mateso yake alitumia machozi alipokuwa anazihakiwa na marafiki zake (Ayubu 10:20) na tunajuwa ya kwamba kisha majaribu; Mungu akashurutisha hao marafiki zake walio mulilisha katika kipindi cha mateso, wamutoleye ngombe na kondoo na awaombeye, ili hasira ya Mungu isiwake ju yao tena;


*    Kuna kilio cha kutubu na kutengeneza maisha mbele za Mungu: Kwenye kitabu cha Luka 7:38, 48; kuna kahaba aliye ingiya ndani ya nyumba ya Mufarisayo aitwaye Simoni; aliye mupokeya Yesu nyumbani kwake, mama huyo alipoingiya akashuka kwenye miguu ya Yesu akamupaka malashi ya samani miguuni huku akilia kwa machozi mengi bila kunena neno lolote; Yesu akasoma siri na haja ya moyo wake na akasemehewa thambi zake zote, bila maombi marefu;


*      Kuna kilio ambacho ni maombi mbele za Mungu: 

·    Mufalme Daudi alitumiya Zaidi sana hayo maombi Zaburi 39:12: “Ee Bwana, usikiye maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyanyamalie machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako.”

·   Nabii Yeremia naye vilevile alinena akisema: “BWANA wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji. Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu. Lakini lisikieni neno la BWANA, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia. Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu. Nena, BWANA asema hivi, Mizoga ya watu itaanguka kama samadi juu ya mashamba, Na kama konzi ya ngano nyuma yake avunaye, wala hapana mtu atakayeikusanya.” (Yeremia 9:17-22);

·  Mungu alimusikiya na ku murehemu Mufalme Hezekiya kwa kuangaliya machozi yake akamwambiya nabii Isaya: “Enenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimesikiya maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziogeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano”. (Isaya 38:5). 

N.B:Machozi ya mcha Mungu yanaonekana mbele za Mungu.

·  Taifa la Israeli utumwani Misri walikumbukwa na Bwana Mungu, kisha kumulilia baada ya myaka mia ine na makumi tatu ya utumwa (soma Kutoka 12:40-41); hapo tayari muda wao wa kuondoka kutoka utumwani umeisha timiya zamani. Walipo liya tu mbele za Bwana, sawasawa na neno la Mungu:“Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia. (Kutoka 2:23-25).

 

*      Kuna machozi yenye uchungu sababu ya kukosa mufariji :

·   Nabii Yeremia aliliya kwa uchungu mbele za Mungu; Israeli walipo pelekwa utumwani nakusema : «Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa! Hulia sana wakati wa usiku, Na machozi yake yapo mashavuni; Miongoni mwa wote waliompenda Hakuna hata mmoja amfarijiye; Rafiki zake wote wamemtenda hila, Wamekuwa adui zake. Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa, Na kwa sababu ya utumwa mkuu; Anakaa kati ya makafiri, Haoni raha iwayo yote; Wote waliomfuata wamempata Katika dhiki yake. » (Maombolezo 1:1-3) ;

· Nabii Yeremia aliliya kwa uchungu ; Israeli walipo kataa kusikiya Neno la Mungu na kupelekwa utumwani : « Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa hali ya kufungwa. Nawe utawaambia neno hili, Macho yangu na yatiririke machozi, usiku na mchana, wala yasikome; kwa maana bikira, binti ya watu wangu, amevunjika mavunjiko makuu, kwa jeraha isiyoponyeka. » (Yeremia 13:17; 14:17)


Kutokana na maelezo hapo juu na kulingana na neno la Mungu katika kitabu cha Ufunuo 7:16-17; inayo sema: “Hawataona tena njaa wala kiu; jua wala joto kali halitawachoma tena, kwasababu Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uzima. Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao."

Inasikika waziwazi ya kwamba hata Mungu mbinguni anafurahi tunapo muliliya kwa machozi sababu ya shida, tena tumesikiya ya kwamba Mungu anaelewa kama kuna machozi ambayo ni lazima wakristo wa kweli waliye hapa duniani kabla ya kunyakuliwa kwa kanisa; sababu Mungu hawezi kufuta kitu kisicho kuweko.

Hata wataalamu wa psychologia wanazoweya kusema kama machozi ina kazi yake ndani ya maisha yetu hapa chini tukiwa na musiba au (trauma). Na hata kitabu cha Muhubiri 3:4; inaeleza kama; vile vile tunatakiwa kucheka kwaajili ya afya yetu wakati wa furaha; vivyo hivyo tunatakiwa pia kuliya kwa ajili ya afya yetu wakati wa kilio au msiba fulani; yaani kicheko kama vile machozi ni dawa; ila ni lazima kila kitu kitendeke kwa utaratibu, kikadirishwe kikitumiwa pamoja na kiasi (moderation).

Kwa mwisho, tukumbuke wakati huu wa mwisho wa mwaka wa 2022 na kutaka kuanza mwaka mupya wa 2023 kwa neema yake BWANA Mungu ; ni vema zaidi kutenga muda wa kuchunguza kwa kufanya (assessment) ili kuangaliya wapi tulikoseya, wapi mambo hayakuendeka vizuri sawasawa na mipango au matarajiyo yetu; nini iliendeka vizuri, sambamba; kisha tujiulize ikiwa tulifanya kila kitu sawa sawa na mapenzi ya BWANA Mungu (yaani tujiswali ikiwa tulifanya kila kitu kwa kuimarisha au kujenga ufalme wa BWANA Mungu hapa chini ya juwa) au labda tulitumika kwa kutafuta faida zetu wenyewe?

Kisha hilo zowezi, kwanini tusishukuru Mungu kwa kutuwezesha kufikiya matokeo mazuri tuliyo pata na kumuomba kwa kutumiya hata machozi yetu; halama ya kutubu; ili aturehemu kwa yale ambayo hatukufikiliya sawasawa na mapezi yake. Na tumuonyeshe mwaka mpya yenye kujaa chagamoto (surprises) nyingi na maswali mengi; ili atusaidiye na kutuwezesha kubadilika kimutazamo na kuachana na mwenendo mubaya ambayo inaweza tupelekeya kukwama ndani ya mipango yetu katika mwaka mpya 2023.


Umenielewa? Ikiwa hujaelewa, tafadhali fuatana nami tena katika mfululizo mwingine wa somo hili, siku chache zijazo. Tuzidi kuombeana.

Ni mimi katika utumishi wa Kristo.

 

 Pasteur Thaddée Bizy Barhazigirandi

UJUMBE WA NENO LA MUNGU KWA WATU WOTE
Umeletwa kwako na:
Kanisa "MULIMA WA MAKIMBILIO" 

Communauté des Eglises Evangéliques pour toutes les Nations-Unies "CEENU"

N° 005, Av. Mulungulungu, Quartier Panzi, Commune of Ibanda, Jiji la Bukavu-DR Kongo

chini ya mita 100 kwenye RN2

Barua pepe: tbizyma@gmail.com, thaddemabize@yahoo.fr 

Simu. : WhatsApp: (+243) 995416144: , +243 818216066.
Facebook: Thaddée Barhazigarndi; Twitter: @ThaddeeBizimana
Linkedin: https://www.linkedin.com/in/thaddée-bizimana-b79301a8

 

Commentaires

  1. Mungu Baba yetu wa mbinguni akupanguze machozi wewe unayeliya kwa wakati huu unaposoma ujumbe huu wa Neno la Mungu. Neno hili liwe faraja kwako !
    Mubarikiwe sana na Bwana wa kazi.

    RépondreSupprimer
  2. Mungu Baba yetu wa mbinguni akupanguze machozi wewe unayeliya kwa wakati huu unaposoma ujumbe huu wa Neno la Mungu. Neno hili liwe faraja kwako !
    Mubarikiwe sana na Bwana wa kazi.

    RépondreSupprimer

Enregistrer un commentaire

Posts les plus consultés de ce blog

KWA NINI MTU MWENYE THAMBI ANAPO AMINI YESU KRISTO, KIPATO CHAKE NI KAMA KINA ZOROTA?

RETOURNEZ VOTRE PREMIER AMOUR CAR NOUS SOMMES AUX DERNIERS JOURS, AFIN DE FINIR VORE COURSE AVEC SUCCES

LE PECHE ET SES CONSEQUENCES DANS NOTRE VIE: