YESU KRISTO AKIJA LEO, JE, ATAIONA IMANI DUNIANI ?

 Maandiko : Luka 18:7-8 ; 22:31-32


Swali hili mara na mara lina nitiya woga sana ninapo soma hizi habari.

Niliposoma kwa makini na kutafakari kuhusu hili swali Yesu alilouliza mitume; ni kawa na maswali pia, na hapo nikatambuwa maneno yafuatayo:

·   Imani ya mukristo inatakiwa ionekane si tu kwa macho ya kiroho ila pia kwa macho ya kimwili yaani mbele za Mungu na mbele za watu :

Ni lazima au muhimu imani ionekane hata kama neno la Mungu kwa kitabu cha Warumi 10:10a inasema : « … Kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, … »  yaani imani ni kitu cha moyoni. Lakini pia Mtume Yakobo anatushauri ya kwamba « …Imani isipokuwa inamatendo, imekufa nafsini mwake ».

Kwa hiyo, mukristo wa kweli anatambulikana hata kwa kumutazama na macho ya inje ; kupitiya tabia yake, matendo na mwenendo wake, masemi, mavaliyo hata hali yake ya kuishi na wengine ; sababu imani kama vile upendo na matumaini vyote ni mambo ya moyoni na ni vigumu kuviona ila inawezekana kwa matendo. Tena ni lazima kujuwa ya kwamba sawasawa na neno la Mungu; hakuna Imani bila Matumaini na Upendo "Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo" (1 Wakorintho 13:13). Kwa hiyo; ni lazima mtu mwenye imani aonekane pia akiwa na matumaini pamoja na upendo. Mtu mwenye Imani bila hayo mambo mengine inamaana haiko imani ya kweli au yenye kumutegemeya Kristo; na Yesu akija duniani hataiona kamwe, sababu ni imani mufu, yaani imekufa.

Tena mukristo yeyote lazima aamini; yaani awe na uhakika ya kwamba : Yesu Kristo ni Mwokozi, Mukombozi, Bwana, tena ni "yeye yule, jana na leo na hata milile" (Waebrania 13:8);  aliyezaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho mutakatifu, akateswa zamani za Pilato, akasulubiwa (kapigwa mijeleti tangu usiku wa siku ya inne hadi siku ya tano saa tisa za muchana, kavikwa taji ya miiba kichwani, kabebeshwa musalaba muzito, katemewa mate usoni, kapigwa misumari miguuni na mikononi, akaangikwa musalabani katikati ya wanyanganyi wa wili, kanyweshwa siki na sifongo, kachomwa mukuki ubavumi maji na damu vikandondoka) ; akafa akazikwa kaburini na siku ya tatu akafufuka ; akapaa mbingini kutuandaliya makao, na atarudi tena siku ya mwisho kuchukuwa walio kufa na walio hai kwenda nao mbinguni, ...

·    Nilitambuwa ya kwamba, Yesu Kristo aliuliza hilo swali kisha kutambua waziwazi ya kwamba siku za mwisho watu wengi watajitenga na Imani ya kweli:

Wakisikiliza na kufuata roho zidaganyazo, na mafundisho ya mashetani soma (1 Timotheo 4:1) ; na hapo upendo wa wengi utapowa soma (Mathayo 24:12); tena Yesu alijuwa kwamba kutakuweko watu wenye Imani ya unafiki (1 Timotheo 1:5). Kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yahana 2:12-13 ; tuna soma : « Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani ». Ninapo soma hii maandiko naongopa sana kwa sababu mambo tunayo yaona na kuishi nyakati hizi za jioni, makanisani ndani ya ofisi (kazini); sokoni; nyumbani na penginepo ; kumbe haiko mapya ; sababu Roho wa Bwana alikwisha kutabiri ju ya watu wenye imani za unafiki ; wanao tumika na kutengemeya musaada wa mapepo na nguvu za giza kwa kufanya miujiza mingi, kwa kijitajirisha, kuinuliwa, kuheshimiwa; na bado wanalitaja na kuliitiya jina la Bwana na kumuamini Yesu (kwa midomo tu; ila ndani ya myoyo yao hakuna tena ushirika naye); sababu tayari wameikana ile imani ya kweli tuliyo itaja hapo juu. Watu hao wanalinganishwa na watu wa siku za mwisho ambao mutume Paulo aliandikiya mtoto wake wa imani Timotheo : « [Watu wa siku za mwisho watakuwa] wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumupenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake ; … » (2 Timotheo 3:4-5) ;

Watu hao ni watu ambao wanamwamini na kumujuwa Mungu ila kwa kweli hawamutegemeyi wala kumutumainiya, na hawamupendi tena. Watu hao hawana tena woga, wala hawatetemeki tena mbele za Mungu; na hawatambuwi tena: Mungu wa mbinguni kama Mungu mkuu, Mungu mwenye wivu, Mungu wa miungu (sababu wana miungu migeni ambayo wanategemeya na kuomba msaada wakati washida); hawatambuwi tena Mungu kama: Mungu muweza yote ; Muponyi apitaye wote ; Mungu aliye karibu nasi kuliko hata pumuzi yetu; Mungu mulinzi asiye lala wala kusinziya; Mungu mwinuwa wanyonge toka mavumbini na kuwaketisha kwenye kiti cha enzi; Mungu aliye mwaminifu sana, asiyebadilika katika mipango wala kusema uongo; Mungu asiye linganishwa wala kufananishwa na chochote. Hapo sasa, wakristo wa kweli wanatakiwa kumomba sana Mungu na kukesha kila siku; sababu Yesu Kristo alitabiri kuhusu dalili za siku za mwisho; ya kwamba siku za mwisho manabii wa uongo watajitokeza na kusema wala kujiita wao njo Kristo (Mathao 24:23-24) ;

N.B : Imani ya aina hiyo ; Shetani hana shida nayo, kwa kuwa siyo tishio kwake !

·    Kwa nini sasa Shetani anawinda sana imani yenye kumutengemeya na kumutumainiya Mungu ?

-    Sababu, imani yenye kumutengemea na kumutumainia Mungu, ni tishiyo sana kwa Shetani, sababu imani ni silaha kati ya silaha za Roho iliyo ya ajabu kwa mukristo, yaani Imani ni ngao yenye kuizima mishale ya moto ya yule Shetani : « zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. » (Waefeso 6:16) ;

- Sababu pasipo imani yenye kumutegemea Mungu, hatuwezi kumupendeza [Mungu] kamwe (Waebrania 11:6) ;

-      Pasipo imani hatuwezi kuona mukono au musahada wa Mungu: Kwangu mimi, nalingalisha Imani na mukono wa binadamu. Kumbuka pia kwamba hata Yesu hakuponya kila mtu ; bali aliwaponya waliyo kuwa na haja ya kuponywa yaani wenye imani ya kumutumaniya na kumutegemeya « Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa. » (Luka 9:11).

 

·   Kwa nini ni bora sana kuiombea imani ?

-     Sababu imani inapimwa sana tena sana, na kipimo chake ni majaribu (Warumi 5:3-5). Tena ni ole sana mukristo ajaribiwe wakati imani yake ikiwa chini sana kadiri ilivyo takiwa, sababu Neno la Mungu linasema : « Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. (1 Wakorintho 10:13) ; Yesu Kristo ka ongeza kusema kwenye kitabu cha Mathayo 17:20 "Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu."

-   Sababu mukristo anatakiwa kwenda imani hadi imani, utukufu hadi utukufu ; yaani imani inatakakiwa kukomaa ; sababu inapimwa mbele za Mungu (Mathayo 8:10);

-     Sababu mtu hawezi pewa: Kusimamiya watu, Mali, Uongozi, jukumu au kazi, cheo, zawadi za rohoni; na bado haja pimwa kama anauwezo wakuvibeba ; ndivyo hivyo imani kwa mukrito ni sawa kibebeo (support) sawasawa na neno la Mungu : « Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani» (Warumi 12:3). Kumbe kuna baraka zingine hatuja pewa na mahitaji mengine hatuja jibiwa, siyo sababu ya zambi, wala kuomba vibaya, wala Sheteni; ila ni sababu, bado Mungu anapotazama kiwango cha imani yetu anakuta bado hatujasitahili wala kukamilika. Sababu "... kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza" (Mithali 1:32).

 - Sababu ingine, ni kwamba wakristo ni lazima waenende na kufanya kila kitu kwa imani wala si kwa kuona wala kutazama kwa macho ya inje. Yaani imani ni kama macho ya mukristo kiroho : "(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)" 2 Wakorintho 5:7

Kwa kumaliza tumesikiya sasa kwamba; ili Yesu Kristo aje na kuiona imani bado inasimama, atakapo rudi ya mara ya pili duniani; kuja kuchukuwa kanisa lake na watakatifu pamoja na wateule wake walio fuwa fazi zao ndani ya damu ya mwana kondoo ; ni bora zaidi kuombea imani yetu kama vile tunavyo ombea mahitaji mengine kila siku bila kukoma; najuwa ya kwamba wakristo waliyo wengi hawana ile desturi ya kuona imani yao inakomala; au ni sababu bado walikuwa hawaja juwa hizi siri; waka zarau na kuona kuwa si kitu cha muhimu ambacho kinatakiwa kuombewa; na kulishwa na kuchochewa sana kila siku; kupitiya kusoma na kusikiliza neno la Mungu kwa kuitafakari; pamoja na sala na dua mbele za Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Yesu Kristo alipo iona kazi kubwa yaani maono ya Mtume Petro ; alimuombea na kuombea imani yake ili isitindike « Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. » (Luka 22:31-32).

Tena neno la Mungu linasema : « Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno. Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. » (Yakobo 1:2-4,12).

 

Umenielewa? Ikiwa hujaelewa, tafadhali fuatana nami tena katika mfululizo mwingine wa somo hili, siku chache zijazo. Tuzidi kuombeana.

Ni mimi katika utumishi wa Kristo.

Pasteur Thaddée Bizy Barhazigirandi

UJUMBE WA NENO LA MUNGU KWA WATU WOTE
Umeletwa kwako na:
KANISA "MULIMA WA MAKIMBILIO" 

Communauté des Eglises Evangéliques pour toutes les Nations-Unies "CEENU"

N° 005, Av. Mulungulungu, Quartier Panzi, Commune of Ibanda, Jiji la Bukavu-DR Congo; chini ya mita 100 kwenye RN2

Barua pepe: tbizyma@gmail.com, thaddemabize@yahoo.fr 

Simu. : WhatsApp: (+243) 995416144, +243 818216066.

Facebook: Thaddée Barhazigarndi; 
Twitter: @ThaddeeBizimana
Linkedin: https://www.linkedin.com/in/thaddée-bizimana-b79301a8

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

KWA NINI MTU MWENYE THAMBI ANAPO AMINI YESU KRISTO, KIPATO CHAKE NI KAMA KINA ZOROTA?

RETOURNEZ VOTRE PREMIER AMOUR CAR NOUS SOMMES AUX DERNIERS JOURS, AFIN DE FINIR VORE COURSE AVEC SUCCES

LE PECHE ET SES CONSEQUENCES DANS NOTRE VIE: